
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga
Push Up na wasanii wa Tanzania One Theatre (TOT) wakati wa sherehe ya
ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019.
Rais
wa Tanzania, John Magufuli leo Alhamisi Agosti Mosi, 2019 amepiga
‘push-up’ tisa kabla ya kuzindua jengo jipya la tatu la abiria katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015, ilikuwa ni kawaida
kumshuhudia Rais Magufuli akipiga ‘push-up’ katika mikutano yake
mbalimbali hali iliyotafsiriwa kuwa yuko imara kuwatumikia Watanzania.
Leo amerudia tena wakati akiongoza viongozi walioketi meza kuu kwenda kuwatunza waimbaji wa bendi ya Tanzania One Theatre (TOT).
Alipofika mbele ya wanenguaji wa bendi hiyo alisimama mbele yao kupiga
‘push-up’ tisa na kunyanyuka hali iliyoibua shangwe kwa waliohudhuria
uzinduzi huo.
Comments
Post a Comment