NMB YAUNGANA NA WADAU WENGINE KUJENGA ZAHANATI

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akimshukuru Meneja wa NMB Tawi la Bukombe Andrew Msonga kwa mchango wake wa mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nampalahara.



Wananchi wa Kijiji cha Napalahara wakishusha saruji iliyoletwa na  Meneja wa NMB Tawi la Bukombe Andrew Msonga ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati.
Diwani wa Kata ya Busonzo Mhe Safari Nikas Mayala akipokea mifuko 10 ya saruji kutoka kwa Meneja wa  NMB Tawi la Bukombe Andrew Msonga.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akishiriki katika ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nampalahara.
Meneja wa NMB tawi la Bukombe Andrew Msonga akishiriki katika ujenzi wa Zahanati.



Hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Zahanti ya Kijiji cha Nampalahara uliosimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba baada ya kupiga kambi kwa siku mbili



 




Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Bukombe Mkoani Geita Andrew Msonga alikabidhi mifuko 10 ya saruji yenye thamani ya Tsh 190,000 baada ya kuona jitihada za serikali ya Wilaya  kuweka kambi ya siku mbili katika Kijiji cha Nampalahara Kata ya Busonzo kwa ajili ya kusimamia ujenzi wa Zahanati.

Msonga alisema amefikia hatua hiyo baada ya kuona jitihada za wadau wengine kama Mhe Doto Biteko na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba pamoja na Wananchi wa Nampalahara kwa namna wanavyojitolea ili kujiletea maendeleo wenyewe.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba alisema ziara yake ya siku mbili ya kusukuma shughuli za maendeleo kwa wananchi na viongozi wa serikali ya Kijiji na Kata kwa kujenga Zahanati ambayo ujenzi wake ulikuwa umelega lega tangu mwaka 2016.

Nkumba alisema hayo wakati akipokea matofari 4000 yenye thamani ya sh 4.8 milioni na mifuko 50 ya saruji yenye thamani ya sh 950,000  kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Biteko kwa lengo la kuunga mkono nguvu za wananchi.

Nae Diwani wa Kata ya Busonzo Mhe Safari Nikas Mayala alisema Kata ina vijiji vitano vitongoji 24 lakini hakuna Zahanati wala Kituo cha Afya hali ambayo imekuwa ikipelekea wananchi kutembea umbali mrefu zaidi ya kilomita 18 kutoka Kijiji cha Nampalahara kwenda Kituo cha Afya Uyovu huku wengine kutoka katika kijiji cha Idoselo wakilazimika kutembea kilomita 24 kwenda kutafuta huduma hiyo ya Afya kwenye Kata jirani ya Uyovu.

Mkazi wa kijiji cha Nampalahala Zakia Jemes  alisema wananchi wanateseka zaidi ya miaka 20 hali ambayo imekuwa ikiwafanya wanawake kuzalia njiani.
 "naishukuru serikali kwa kuja hapa kwa  siku mbili kusimamia ujenzi huu utatusaidia kukamilika kwa haraka kwa ujenzi huo na hatimae kuanza kupata huduma hiyo hapa karibu"Alisema Zakia.

Comments