Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe.
Jenista Mhagama
TIMU ya Kilimahewa fc ya
kata ya Katente tarafa ya Ushirombo wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita, imetwaa kwa
mara ya kwanza ubingwa wa ligi ya Doto Cup 2019 kwa kuichapa timu ya Runzewe
Academy goli 2-1 katika faina iliyofanyika katika uwanja wa kilimahewa.
Mfungaji wa magoli ya timu
ya Kilimahewa fc Fc Hamis Julius
aliwanyanyua mashabiki wake baada ya kuingiza kimiani bao la kwanza dakika ya
62 na dakika ya 67 aliongeza bao lingine hadi ambali lilidumu hadi kipenga cha
mwisho.
Mfungaji wa goli la timu ya
Runzewe Academy lilifungwa na Rashidi Sanga dakika ya 13 ambalo lilidumu na
kuwa la kufutia machozi timu hiyo ilisha wahi kuchukuwa ubingwa wa Doto Cup
misimu miwili 2016 na 2017 mwaka 2018 kombe hili lilichukuliwa na timu
Ushirombo Rengezi 2019 limebaki mjini
tena Kilimahewa fc.
Mdhamini wa mashindano bunge wa Jimbo la Bukombe pia
waziri wa Madini Doto Biteko katika hafla ya kukabidhi zawadi za washindi
aliwasii vijana wa timu 165 zilizoshiriki
katika mashindano hayo yaliyozinduliwa Julai 5 mwaka huu na kufika
tamati Agosti 24 kuhakikisha kuwa wanaendeleza vipaji vyao vilivyoibuliwa na kutumia fursa hiyo kupata
ajira.
“Kupitia ligi hii timu zilizoshiriki ni 165
walioshinda na walioshinda wote muwe wamoja katika kuendeleza urafiki
na vipaji ambavyo niajira,” Alisema Biteko.
Mgeni rasmi Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri mkuu, (sera,
Bunge, kazi, ajira na wenye ulemavu) Jenista Mhagama alisema kuwa iwapo vijana
watafuata kanuni, taratibu na sheria za mpira wa miguu kazi hiyo ni ajira rasmi
siyo ya kubezwa.
Mhagama licha ya kumpongeza Mbunge Biteko alisema kuwa
ligi hiyo ya Doto Cup kama itaendelezwa vijana wanaweza kuepukana na vishawishi
vya kujiunga na makundi mabaya kama ya uvutaji wa madawa ya kulevya hali ambayo
itapelekea kupata magonjwa mengine ya kuambukiza kama UKIMWI.
Katika hafla hiyo pia
Mhagama aliweza kukabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza Kilimahewa Fc
kiasi cha shilingi Milioni 1, mipira mitatu na jeshi seti tatu huku mshindi wa
pili ambaye ni Runzewe Academy alikabidhiwa shilingi 500,000, mipila miwili na
jezi seti mbili na mshindi wa tatu Sinamila FC alikabidhiwa shilingi 200,000 na
mpira mmoja huku Chui Fc mambaye ni mshindi wa nne aliambulia seti moja ya jezi
na mpira mmoja.
Kauri mbiu ya ligi hiyo ilikuwa ni “Kusema na kutenda.
Comments
Post a Comment