KANAL LUBINGA AWATAKA VIONGOZI WA CCM KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA CHAGUZI


Katibu wa Nec siasa na uhusiano wa kimataifa CCM Kanali  Ngemela Lubinga akizungumza na viongozi wa ccm kuanzia ngazi ya Matawi hadi Wilaya-Bukombe.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukombe Daniel Machongo akizungumzana viongozi wa ccm kuanzia ngazi ya Matawi hadi Wilaya-Bukombe.

Mbunge Wa Jimbo la Bukombe Mhe.Doto Mashaka Biteko akizungumza na viongozi wa ccm kuanzia ngazi ya Matawi hadi Wilaya-Bukombe.


Mbunge Wa Jimbo la Bukombe Mhe.Doto Mashaka Biteko akiwa ameshikilia cheti cha pongezi kutoka kwa uongozi wa CCM Wilaya-Bukombe na kukabidhiwa na Katibu wa Nec Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Kanali  Ngemela Lubinga
 

 Viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya Matawi hadi Wilaya wakiwa ukumbini.
Viongozi wa Dini na Wazee maarufu wakiwa ukumbini.

Katibu wa Nec siasa na uhusiano wa kimataifa CCM Kanali  Ngemela Lubinga  amewataka viongozi wa chama cha mapinduzi CCM kuanzia ngazi ya matawi kuhakikisha wanahamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwa zoezi hilo linatalajiwa kuanza uboreshaji huo Agost 26 serikali inaanza kuboresha daftari hilo ili wananchi waliofikia umri wa miana 18 wawe na haki ya kuchagua kiongozi wanae mtaka.

Lubinga aliyasema hayo wakati akizungumuza na viongozi wa CCM ngazi ya matawi hadi wilaya  kwenye mkutano  kwa lengo la kuimarisha chama uliofanyika Wilayani Bukombe na kuhudhuliwa na viongozi wa Wilaya na Mkoa wa Geita kwa lengo la kupokea maelekezo ya chama ngazi ya Taifa.

Alisema mwaka  2015 Tanzania ilikuwa na vituo vya Afya  115  lakini kwa kutekeleza ilani ya CCM  hadi  sasa serikali ya awamu ya tano kuna vituo vya Afya 353.

Lubinga alisema serikali kila mwezi inatoa Tsh Bilion 24  kwa ajili ya kuhudumia Elimu Bure kaptesheni za shule ya msingi na sekondari  kwa  huku mikopo chuoni  serikali kila mwaka inatowa sh 480 bilioni kwa ajiri ya mikopo wanafunzi wa chuo naserikali inatalajia kununua ndege zingine.

Mbuge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko ambae pia ni Waziri wa Madini aliwaomba viongozi wa chama kuacha makundi badala yake watimize wajibu wa kuwahudumia wananchi ili washiriki vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa zitakazo fanyika Oktoba mwaka huu.

Comments