Timu 6 kati ya nane zinazotarajia
kuingia hatua ya fainali ngazi ya Tarafa katika Mashindamo ya Mpira wa Mguu
kombe la Dotto Cup 2019 wilaya ya Bukombe mkoani Geita zimefuzi kuingia katika
hatua hiyo baada ya kuibuka na ushindi kwenye hatua ya mashindano ngazi ya
tarafa.
Mashindano hayo yalianza kutimua
vumbi Julai 8, mwaka huu yakishirikisha jumla ya Timu 165 kutoka ngazi ya
kijiji na jumla ya Timu 17 ziliingia katika hatua ya fainali ngazi ya Tarafa.
Ligi hiyo imeingia hatua ya fainali
ngazi ya Tarafa na kwamba kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu
wilaya ya Bukombe (BUFA) Bosco Mwidadi timu zilizofuzu kuingia hatua hiyo baada
ya michezo Minne iliyofanyika katika Viwanja vya Ushorobo kati ya Timu ya
Kilimahewa FC iliyoibuka na ushindi wa Mabao 3-1 dhidi ya wenyeji timu ya
Bukombe United.
Katika Uwanja wa Tarafa ya Bukombe Timu ya
Chui FC imeichapa 3-1 Timu ya Iyogelo FC,Uwanja wa Uyovu Timu ya Namonge FC
imeibuka na ushidi wa bao 1-0 dhidi ya Namsega FC,na katika Tarafa ya Kisoka
Timu ya Sinamila FC imeibuka na Ushidi wa mabao 2-0 dhidi ya Miyenze FC.
Mwidadi amezitaja timu ambazo zitacheza
fainali ngazi ya tarafa Julai 5 mwaka huu kutafuta bingwa kwa kila tarafa ni
timu ya NGM FC itakutana na Sinamila fc katika uwanja wa Bulega huku timu ya
Bukombe star itakutana na timu ya Chui fc zitacheza katika uwanja wa Bugelenga
na timu ya Ushirombo Worrios itachuwana na timu ya Kilimahewa fc uwanja wa Ushirombo
mjini katika tarafa ya Siloka bado mashindano
yanaendelea kutafuta timu mbili zitakazo ingia fainali hiyo.
Mwidadi amesema kwamba mashindano
hayo yanadhaminiwa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye ni Waziri wa Madini Doto
Biteko lengo likiwa ni kuibua,kuendeleza,na kukuza vipaji vya soka wilayani hhapa pamoja na kujenga
mahusiano mema kwa jamii ya wilaya hiyo.
Fainali ya mashindano hayo inatarajia
kufanyika Agosti 10 au 12 ,mwaka huu kwa kutegemea karenda ya mdhamini wa
mashindano.
Comments
Post a Comment