Mahakama ya Hakimu mkazi Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita,imemuhukumu kwenda kutumikia adhabu ya
kifungo cha maisha jela mkazi wa kijiji cha Lyobahika kata ya Uyovu Tarafa ya
Siloka Ruben Maiko (19) kwa kosa la
kumbaka mtoto wa umri wa miaka mitatu.
Hakimu mkazi Mahakama ya Wilaya ya
Bukombe Amon Kahimba akitoa hukumu hiyo alisema mshtakiwa alitenda kosa la
ubakaji majira ya saa 1:00 jioni Agosti 8 mwaka 2019 kijiji cha Lyobahika akiwa nyumbani kwa Doto
Wiliamu anaedaiwa kuwa mpenzi wake na mama wa mtoto aliye bakwa.
Mshtakiwa aliingia chumbani akamuita mtoto
chumbani na kumbaka kisha kumusababishia maumivu makali sehemu ya mwili wake baada ya kumkuta mama wa mtoto
huyo hayupo ameenda kwenye majukumu yake.
Kahimba alisema kutokana na ushahidi
uliotolewa na upande wa mashitaka mahakamani hapa na vielelezo vya madaktari na
upande wa Doto Wiliamu mama mzazi wa mtoto na mashuuda wengine ushahidi ambao
hauja acha shaka mahakamani.
Kutokana na kosa hilo mshtakiwa ataenda
kutumikia kifungo cha maisha jela ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ovu
ya kutenda kosa kama hilo.
Mshitakiwa Ruben Mariko akitowa
utetezi wake mahakamani hapo aliomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa
kutoisumbua alikili kutenda kosa hilo na kuongeza kuwa alikuwa na mahusiano ya
kimapenzi na mama wa mtoto huyo alifika nyumbani hapo akamkuta mpenzi wake
amekwenda kuhudumia bar ndipo akambaka mtoto wa mpenzi wake.
Awali mwendesha mashtaka wa polisi Neema
Nhaluke aliomba mahakama kutowa adhabu kali kwa mshtakiwa kutokana na vitendo
vya kubakwa watoto vimekuwa vikitokea
mara kwa mara Wilayani hapa.
Comments
Post a Comment