Watu
watatu raia wa kigeni kutoka nchi za Ireland na Uingereza wamepandishwa
kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za
kupatikana na madini aina ya dhahabu yenye thamani ya zaidi ya shilingi
Milioni 98 kinyume na sheria na taratibu za nchi.
Akisoma
Shtaka Mwendesha Mashitaka wakili Msomi wa Serikali Mwandamizi
Jacqueline Nyantori, anasema washtakiwa hao kwa pamoja wametenda kosa
hilo la uhujumu uchumi July 3, 2019 na kukamatwa katika uwanja wa Ndege
Songwe uliopo Mkoani Mbeya ambapo walikutwa na madini aina ya yenye
uzito wa gram 1043.33 yenye thamani ya shilingi milioni 98.5 .
Wakili
huyo amewataja washtakiwa hao kuwa ni Clive Rooney (62) raia wa Irish
ambaye ni Meneja wa fedha, Ross Harris (34) na Robert Wheedon (59)ambao
ni raia wa Uingereza ambapo wamekamatwa na madini hayo wakiyasafirisha
kuelekea Jijini Dar es Salaam.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali amesema washtakiwa hao wamekamatwa na Madini
kinyume cha Sheria ya Uhujumu uchumi namba 18 (1) na 4 kifungu cha (1a)
na kifungu cha sheria ya madini namba 14 cha mwaka 2010, ikiwa ni pamoja
na aya ya 27 ya jedwali la kwanza na kifungu namba 57 kifungu kidogo.
Aidha
Kaimu Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya Venance
Mulingi amesema Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shtaka hili
ambapo washtakiwa wamerudishwa wamerudishwe rumande hadi July 22 mwaka
huu.
Comments
Post a Comment