WANANCHI WACHANGISHANA KUJENGA ZAHANATI

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto M. Biteko akizungumza na Wananchi

Wananchi wa Kijiji cha Sinamila Kata ya Butizya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, wameanza kuchangishana ili kujenga Zahanati ya kijiji ili waondokane na changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za Afya.
Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Bukombe Daniel Machongo akizungumza na wananchi 






Hayo yalielezwa na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Silamira Aly Maganga kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko akihimiza maendeleo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Butinzya Amos Shimo alimshukuru sana Mbunge kwa jitihada zake za kuleta maendeleo sambamba na kuahidi kushirikiana nae bega kwa bega ili kuharakisha maendeleo ya Butinzya na Bukombe nzima kwa ujumla. 

Diwani wa Kata ya Butinzya Amos Shimo akizungumza na wananchi
Mbunge wa jinbo la Bukombe Doto Biteko akihamasisha wananchi kuchangia miradi ya maendeleo aliwaunga mkono wananchi kwa kuchangia sh 3 milioni kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati.
Biteko aliwaomba wananchi kuachana na siasa nyepesi zinazopinga maendeleo  badala yake washirikiane kwa kuijenga Bukombe ambapo watoto wakikua waikute Bukombe  ya tofauti  na yenye mabadiliko makubwa  ya kimaendeleo.

"Hakuna maendeleo yanayoweza kuletwa na serikali bila nguvu za wananchi kutangulia ili wananchi kupata huduma bora za afya kila kijiji inatakiwa wananchi kuwa tayali kuchangia" Alisema Biteko.

Comments