USHIROMBO WORIAZ WAIPIGA MSINDIKWA FC 3-0 NGAZI YA TARAFA

Mashindano ya Doto Cup 2019 ngazi ya tarafa yameaza kutimua vumbi timu ya Ushirombo worianzi toka kata ya Bulangwa ameipinga timu ya Msindikwa fc 3-0 toka kata ya Ushirombo.
Wafungaji wa timu ya Ushirombo woriazi Bahati Songoma dakika ya 23 goli la pili lilifungwa na Juma Bokasa dakika ya 55 na goli la tatu limefungwa na Juma Bokasa dakika ya 76.
Kocha wa timu ya Ushirombo woriazi Joseph Kabote amesema kikosichake kiko imala na kwamba vijana katika mshezo wao hawakumfurahisha sana make anawajuwa wako vizuri.
Kabote ameongeza kuwa walibeba ubingwa wakata na watarafa ya Ushirombo wataubeba ili wakatafute ubingwa ngazi ya Wilaya.
Kocha wa timu ya msindikwa fc Wiliam Julius amesema asiekubali kushindwa simusindani na kwamba anamshukuru mungu wachezaji wake wametoka wazima na wamecheza vizuri watajipanga tena mwaka kesho.
Katibu wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Bukombe Bosco Mwidadi amesema katika uwanja wa tarafa ya kimichezo Bulega Nsagal fc imeichapa Roma fc 6-4 kwa njia ya mikwaju ya penaliti.
Mwidadi amesema katika uwanja wa tarafa ya Siloka katika kijiji cha Ikuzi kata ya Rungewe mashariki timu ya Academy fc imepewa pointi tatu baada ya timu ya Makilikili fc ya Ikuzi kushindwa kufika uwanjani.

Amesema  katika mashindano ya tarafa ya Bukombe timu ya Small tiger ya kata ya Lyambamgongo imepigwa na timu ya Bukombe star fc goli 4-1 kwa njia ya penaliti dakika 90 za mchezo ziliisha bila bila.
 Mwidadi amesema mashindano ngazi ya tarafa yanaendelea kutimua vumbi viwanja vya tarafa nne Bukombe, Ushirombo na Siloka, na tarafa nyingine ya kimichezo Bulega.
Amesema mshindi wa kwanza kitarafa atapata zawadi ya seti ya jezi moja na mpira thamani ya sh 125,000 kitita cha fedha cha sh 100,000 mshindi wa pili wa tarafa atatoka na zawadi ya mpila mmoja wenye thamani ya sh 50,000 nakitita cha fedha sh 50000.


Comments