Ununuzi wa zao la Pamba wilayani Kahama wafanyika kwa kusuasua licha ya soko lake kufunguliwa May 5 mwaka huu.
Makampuni
yaliyopewa leseni za kununua zao la pamba katika wilaya ya kahama
mkoani Shinyanga yametakiwa kununua zao hilo kwa wakulima kwa wakati ili
kutoa fursa ya maandalizi ya msimu ujao.
Kauli
hiyo imetolewa na Emmanuel Kileo Mkaguzi wa Pamba wilaya ya kahama
wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana namna
soko la zao hilo linavyoendelea baada ya kuzinduliwa may 5 mwaka huu.
Amesema
kampuni nne zilizopewa leseni ya kununua zao hilo zimekuwa zikinunua
zao hilo kwa kusuasua na kusababisha wakulima wengi kulalamikia namna
masoko ya zao hilo unavyofanyika na yanatakiwa kununua kwa bei elekezi
ya shilingi elfu moja na mia mbili.
Amefafanua
kuwa mpaka sasa kampuni mmoja pekee ya Fresho ndio imeweza kununua
pamba za wakulima kwa kiwango kidogo huku makampuni mengine yakiwa
hayajaanza ununuzi wa lincha ya msimu wa zao hilo kuzinduliwa.
“Wakulima
wetu wamehamasika kulima zao hili na mwaka huu tunatarajia kupata kilo
milioni 4 na laki saba ilikiganishwa na mwaka jana ambapo walilima kilo
milioni 2 na laki tatu”alisema Kileo.
Hata
hivyo Kileo amesema kwa ukaguzi ambao ofisi yake imeufanya wamebaini
pamba yote ni safi na haijachanganywa na maji na kuwataka wakulima
kuzingatia sheria na taratibu za utunzaji wa zao ili ili kupata manufaa
zaidi wanapoifikisha sokoni.
Kampuni
ambapo zimepewa leseni hizo ni pamoja na Fresho, kahama oil mills,
Kahama Cotton Company Limeted na Africian lakini kampuni ya fesho ndio
imeweza kununua pamba pekee ambapo imenunua katika vijiji 46 kati ya 148
vinavyolima zao la Pamba.
Comments
Post a Comment