Tanzania yadhamiria kupunguza matumizi ya Zabaki kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kwa asilimia 30% ifikapo 2024.
Katika
kikao cha kupitisha Mpango Kazi wa Taifa wa kupunguza matumizi ya
Zebaki kwa wachimbaji wadogo kilichoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais
na kushirikisha sekta husika, jana katika Chuo cha Biashara (CBE) jijini
Dodoma, Ikiwa sehemu ya Maandalizi ya utekelezaji wa Mkataba wa
Kimataifa wa Minamata ambao Tanzania ipo kwenye mchakato wa kuridhia.
Zebaki
imetajwa kuwa moja kati ya kemikali kumi hatarishi zilizo orodheshwa na
Shirika la Afya Duniani na ina madhara makubwa haswa kwenye magonjwa ya
mfumo wa fahamu.
Tanzania
inakadiriwa kuwa na wachimbaji wadogo milioni 1.2, asilimia 20-30 ni
wachimbaji wanawake ambapo sehemu kubwa ya wachimbaji hawa hutumia
zebaki huku kukiwa na makisio ya mwaka ambapo tani 13 mpaka 24 hutumika
na huingizwa nchini kinyemela.
Zaidi
ya 25-33% ya wachimbaji wadogo wadogo wameathirika na matumizi ya
zebaki,hivyo Serikali imedhamiria kupunguza ama kuondosha matumizi ya
zebaki kwa wachimbaji wadogo.
Wakizungumza
mara baada ya kumaliza kikao hicho Bi. Noela R. Magoche ambaye ni mdau
wa Madini alisema kuwa zifikiriwe mbinu mbadala kunusuru watoto
wanaofanya kazi migodini kwani ndio waathirika wakubwa wa zebaki huku
akisisitiza sheria inayokataza ajira kwa watoto
Kwa upande wake mdau wa Mazingira Bw. Haji Rehani amesema zebaki imetambulika kimataifa kwa madhara makubwa ya kiafya.
Comments
Post a Comment