TANAPA yaeleza fursa za Utalii mikoa ya Kusini, Magharibi na Kaskazini Magharibi

Kamishna wa Uhifadhi wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Dkt. Allan Kijazi akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa TANAPA, Wahariri na Wanahabari Waandamizi, jana Julai 04, 2019 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akitoa salamu zake kwenye mkutano huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
Mgeni rasmi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala akifungua mkutano huo wa siku mbili kuanzia jana.
Washiriki wa mkutano huo.
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na washiriki wa mkutano huo.
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na washiriki wa mkutano huo wenye lengo la kuimarisha mahusiano baina ya TANAPA na vyombo vya habari katika kuhamasish Utalii na Uhifadhi Tanzania.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwala alipowasili ofisini kwake.
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imebainisha kuelekeza nguvu zaidi katika kutangaza fursa za utalii zilizopo katika ukanda wa Kusini, Magharibi na Kaskazini Magharibi mwa Tanzania hatua itakayosaidia kuongeza idadi ya watalii pamoja na pato la Taifa.

Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Dkt. Allan Kijazi aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa TANAPA, Wahariri na Wanahabari Waandamizi unaofanyika jijini Mwanza.

Itakumbukwa ukanda wa Magharibi mwa Tanzania unahusisha vivutio vilivyo katika mikoa ya Rukwa, Katavi, Kigoma na Tabora huku ukanda wa Kaskazini Magharibi ukihusisha mikoa ya Mwanza, Mara, Geita na Kagera. Aidha ukanda wa Kusini unahusisha mikoa ya Mtwara, Lindi na Mbeya.

Comments