Timu ya Small Tiger Fc
ya Lyambamgongo imeibuka kidedea kwenye Lingi ya Doto Cup 2019 ngazi ya Kata
baada ya kuilaza timu ya Kagwe fc kwa goli 3-2.
Wafungaji wa magoli ya
Small Tiger Fc John Nyahiti dakika ya 15 na Greyson Mtingwa kufunga magoli
mawili dakika ya 42 na ya 52.
Magoli ya timu ya Kagwe
fc yalifungwa na Kashinje Joseph dakika ya 10 na Mathias Charles dakika ya 36.
Aidha Diwani wa Kata ya
Lyambamgongo Boniphance Shitobelo ambae alikuwa mgeni rasmi katika kukabidhi
zawadi za washindi wa kata hiyo ambazo ni seti moja ya jezi na mpira mmoja kwa
mshindi wa kwanza, mshindi wa pili Kagwe
fc walipewa mpira mmoja.
Shitobelo akikabizi
zawadi alisema katika kata hiyo kulikuwa na timu nne zilizoshiriki katika
mashindano hayo Small tiger fc, Ifunde fc, Kagwe fc na Ishololo fc ikiwa timu
iliyo shinda ngazi ya Kata ni Small tiger fc na ushindi huo itaenda kukutana na
timu nne mabingwa wa Kata zingine ngazi ya Tarafa ya Bukombe.
Shitobelo aliwataka
wachezaji kuwa na ushirikiano na timu zilizo shindwa ilikuongeza nguvu na
kutwaa ubingwa kwa ngazi inayofuata
Kwa upande wake nahodha
wa Timu ya Small Tiger Fc John Nyahiti alianza kwa kumshukuru Mbunge wa Jimbo
la Bukombe Doto Mashaka Biteko kwa uamuzi wake wa kuwaunganisha vijana ki
michezo na kuwashukuru wachezaji wenzake kwa kuwa na ushirikiano hadi wameibuka
mabibwa wa Kata huku wakiwahahakishia mashabiki wao kutwaa ubingwa wa Doto cup
2019 katika ngazi ya Wilaya naye nohodha wa timu ya Kagwe fc Ngusa Sameke
alisema mchezo ulikuwa mzuri na kwamba haya matoke wameyapokea vyema.
Katika kiwanja cha
michezo Kata ya Iyogelo kwa mjibu wa msimamizi wa fainali ngazi ya Kata Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Miguu Mkoa wa Geita (GEREFA) Joseph Kabote alisema Timu
zilizoshiriki kwenye Kata hiyo ni Iyogelo Fc, Shibingo Fc, Bugando Fc, Nyamakunkwa
Fc.
Kabote alisema katika
fainali hiyo timu ya Iyogelo Fc imeibuka bigwa wa Kata baada ya kuichapa timu ya
Shibigo Fc goli 9-8 huku timu hizo mbili zilicheza na kutoka sale ya moja kwa
moja na kuingia kutega matuta.
Comments
Post a Comment