Na Amiri kilagalila-Njombe
Serikali
mkoani Njombe imesema imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya bil 1.2
kwa vikundi 561 vya wanawake ,vijana na walemavu katika mwaka wa fedha
2018/2019 ambayo hutolewa kila mwaka na halmashauri kutokana kwenye
asimilia 10 ya mapato ya ndani.
Akizungumza
katika kikao cha halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe
mkuu wa mkoa huo Christopher Olesendeka amesema serikali imeendelea
kurahisisha mazingira ya wajasiriamali na biashara kwa ujumla kwa
kuendelea kuhamasiaha uwekezaji na kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa
vikundi vya ujasiriamali kwa lengo la kukuza mitaji yao.
Mbali
na mikopo Olesendeka pia amesema katika mwaka wa fedha ulioisha juni
serikali imefanikiwa kutekeleza ilani ya chama katika utekelezaji wa
miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuanza ujenzi wa miradi mikubwa
ya barabara zote zinazounganisha wilaya , maji, elimu pamoja na utoaji
wa fedha na miradi kwa kaya masikini kupitia mpango wa TASAF hatua
ambayo imehimarisha huduma na maisha kwa wakazi wa Njombe.
"Kwa
upande wa wanawake ndio waliochangamka sana kuchukuwa mgao wao,jumla ya
sh.milioni770,64 elfu na 91 imechukuliwa na vikundi vya akina mama
vipatavyo 394,tumejitahidi kuwanyang'anya wapinzani ajenda na ukiangalia
kwenye hotuba yangu kwa mkoa wa Njombe zaidi ya bil.480 imetengwa kwa
ajili ya miradi mikubwa ya barabara ya kuunganisha wilaya zetu na makao
makuu ya mkoa"alisema Olesendeka
Akizungumzia
maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi mkoa wa Njombe Jasel Mwamwala ameagiza viongozi na wanachama
wote kujipanga ili kiweze kuibuka kidedea.
"Serikali
za mitaa tukifanya vizuri basi 2020 tutafanya vizuri zaidi, kwa hiyo
niwatake wote jinsi tulivyoagizana kila mmoja akatekeleze kwa umakini
anavyotakiwa akatekeleze"alisema Mwamwala
Comments
Post a Comment