
Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema tangu kuanzishwa kwa kikosi kazi
cha kupambana na ujangili mwaka 2016 idadi ya wanyama hapa nchini
imeongezeka.
Magufuli amesema hayo leo Jumanne Julai 9 mwaka 2019 wakati wa uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato mkoani Geita.
"Mwaka 2014 kulikuwa kuna tembo 43,330 lakini hivi sasa baada ya
kuanzisha kikosi cha kupambana na ujangili wamefikia zaidi ya 60,000
faru hawakuwepo kabisa ila sasa wamefikia 163 hatuna budi kumshukuru
Faru Rajabu mtoto wa Faru John," amesema Magufuli.
"Inaonekana yule Faru wajina wangu (John alikuwa hajitumi vizuri) huyu
mtoto wake nimeambiwa mpaka sasa amekwisha zalisha 43," amesema Rais
Magufuli huku akitabasamu.
Comments
Post a Comment