Waziri
wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dokta Harrison Mwakyembe
ameziagiza idara za kisekta kwa Pande zote mbili za Muungano
kuunganisha nguvu katika kueneza Lugha ya Kiswahili kwa Mataifa
Mbalimbali.
Dokta
Mwakyembe amesema hayo jana Julai 2,2019 jijini Dodoma katika kikao
cha Ushirikiano baina ya Wizara ya Habari ,Utamaduni ,Sanaa na
Michezo pamoja na Serikali ya Mapinduzi ,Zanzibar hususan katika masuala
ya sanaa,Utamaduni ,na Habari.
Waziri
Mwakyembe amesema lengo la kikao hicho ni kujadili Masuala ya Muungano
katika sekta ya Habari na kubadilishana Ushirikiano na uzoefu ambapo
pia wamepokea taarifa ya Makatibu wakuu juu ya Ushirikiano wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivyo,Dokta
Mwakyembe amesema mahitaji ya Lugha ya Kiswahili katika mataifa
mbalimbali ya ulimwengu ni mkubwa ni wakati sasa serikali zote za
Muungano zikajipambanua vyema katika ushirikiano wa kueneza lugha hiyo.
Katika
hatua nyingine Dokta Mwakyembe ameyaagiza shirika la Umma la
Utangazaji Tanzania [TBC] na Shirika la Umma la Utangazaji
Zanzibar,[ZBC] Kuwa na ushirikiano wa Pamoja katika Uzalishaji wa
Vipindi vya runinga ya Taifa ya Utalii,Safari Channel ili kutangaza
utamaduni ,mali kale na vivutio vilivyopo Tanzania kwa ustadi mkubwa
hali itakayosaidia kukuza utalii hapa nchini.
Pia
katika maafikiano ya mkutano huo Waziri Mwakyembe amesema pande zote
mbili za muungano zitashiriki katika maandalizi ya tamasha kubwa la
utamaduni Afrika Mashariki litakalofanyika Mwezi Septemba Jijini Dar
Es Salaam huku mapendekezo mengine ya mkutano huo ni idara zote za
kisekta kushiriki pamoja katika maandalizi ya bajeti kuwezesha timu ya
taifa inaposhiriki mashindano mbalimbali ya Kimataifa.
Sekta
ambazo zimeshiriki katika mkutano huo wenye lengo la kukuza
utamaduni,Sanaa ,Habari na Lugha ya Kiswahili ,ni sekta ya
utamaduni,Sekta ya Utalii,Sekta ya Habari na Sekta ya Sanaa na Michezo.
Comments
Post a Comment