MBUNGE DOTO AWAPIGA JEKI WANANCHI WA KATA YA KATENTE

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe, Doto Mashaka Biteko ambae pia ni Waziri wa Madini akikabidhi fedha kwa Diwani wa
Kata ya Katente Mhe. Bahati Kayagila kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati
 
  Diwani wa Kata ya Katente Mhe Bahati Kayagila akiwaonyesha wananchi fedha baada ya kukabidhiwa na Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb)

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe, Doto Mashaka Biteko akizungumza na wakazi wa Katente

 Diwani wa Kata ya Katente Mhe Bahati Kayagila akizungumza na wakazi wa Katente.
 
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe, Doto Mashaka Biteko baada ya kupokea zawadi ya asali kutoka kwenye uongozi wa Kata ya Katente


Wananchi wa kata ya katente wakimskiliza Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko .

  


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoa wa Geita Doto Mashaka Biteko ambae pia ni Waziri wa Madini amewaunga mkono wananchi wa kata ya Katente Wilayani hapo kwa kutoa milioni 4.8 kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati.

Biteko katika uchangiaji huo ametoa mifuko 100 ya saruji yenye thamani ya sh 1.8 milioni kwa ajili ya kuongeza nguvu ya ujenzi wa Zahanati kijiji cha Bwenda na milioni tatu kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Bomani.

Awali Afisa Mtedaji wa Kata ya Katente Issa Shaban kutoa taarifa kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge wakati wa ziara yake kata ya Katente.
Shaban alisema wananchi wamechangia sh milioni 4 na kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati na kubainisha kuwa wananchi wanapata huduma za Afya kwenye hospitali ya Wilaya.
.
Kwamjibu wa Diwani wa Kata ya Katente Bahati Kayangila alisema wananchi wamechagia sh milioni 6 huku awali Serikali ilitoa Sh milioni 8 na kujengwa hadi hatua ya reta na wananchi kusubili serikal iwasaidie ukamilishaji wa jengo hilo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko aliwaomba wananchi kuhakikisha wanashirikiana kwenye miradi ya maendeleo ili kuijenga Wilaya ya Bukombe.

Biteko alisema wakati wa siasa bado na kwamba kazi yake ni kuhamasisha maendeleo na kuchangia nguvu za wananchi ambao wako tayali kuibuwa miradi kwa kuchangishana na kujitolea nguvu zao.

Comments