Michuano ikiwa inaendelea kati ya Mapinduzi Fc Vs Kadis Fc katika viwanja vya shule ya msingi igulwa
Timu ya Mapinduzi fc ya Katente imeichapa magori 3-1 timu ya
Kadis fc ya bomani katika michezo ya lingi ya Doto Cup 2019 uwanja wa shule ya
msingi Igulwa kata ya Katente wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita.
Mchezaji wa timu ya mapinduzi fc Aron Peter alijifunga goli
moja dakika ya 22 baada ya muda mchache kupachika gori timu ya Kadis fc dakika
ya 13 huku goli lapili timu ya Mapinduzi fc lilifungwa na Mathew Mabenga dakika
ya 54 goli la tatu lilifungwa na Salumu Salum dakika ya 58.
Mchezaji wa timu ya Kadis fc Maganga Paschal alipewa kati
nyekundu kwa kosa la kumudanganya mwamzi wa mchezo huo Projestus Luta kuwa ameumia
akigalagala chini kwa kupoteza muda huku akiwa na kadi ya njano. 
Luta alisema kwa sheria za mpira wa miguu mchezaji huyo haluhusiwi kucheza mechi tatu atakuwa ndani ya adhabu.
Mchezaji huyo Maganga Paschal akizungumzia kupewa kadi
nyekundu alisema hakuwa na talajio ya kupewa kadi nyekundu na hakufanya kosa
kwamakusudi kunakitu kilimfanya kulala kutokana na kuumia gafra.
Alisema hakuna namuna atatumikia adhabu aliyopewa anaiombea
timu yake isitolewe kwenye michezo miwili iliyoko mbele ili ajumwike nao
kuhakikisha wanatafuta ushindi wa kwanza kati ya timu zinazoshiriki mashindano
ya Doto Cup
.

.
Mkazi wa Katente Lazaro Machibya alimpongeza mbunge wa jimbo la Bukombe Doto Biteko kwa kudhamini mashindano ya mpira wa miguu kila mwaka hali ambayo imekuwa ikiwafanya wapenzi wa michezo kufurahi kutokana na kutokuwepo mashindano mala kwa mala ya mpira wa miguu.
Comments
Post a Comment