MAKIRIKIRI FC YAVAA TAJI LA USHINDI DOTO CUP NGAZI YA KATA


Ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya Doto Cup 2019 Timu ya Makirikiri Fc ya Ikuzi Kata ya Runzewe Mashariki Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita, imetwa ubingwa ngazi ya Kata katika mashindano ya fainali ligi ya Doto Cup 2019 kwa kuichapa timu ya Nampangwe fc goli 2-1.
Magori ya timu ya Makirikiri Fc yaliwekwa wavuni na Vitina Kabili  dakika ya 11 na dakika ya 50
Na mfungaji wa gori la Nampangwe fc lilifungwa na Bundala Heriman dakika ya 84.

Katika mchezo huo Pia nahodha wa timu ya Nampangwe  Mawazo Yohana amesema kuwa matokeo ya kushindwa wameyapokea na kwamba ni matokeo ya mchezo.
Yohana aliwaomba wachezaji wa timu ya Makirikiri fc kuendelea kuwa na ushirikiano ili wachukuwe ubingwa wa Tarafa ya Siloka.

Upande wake nahodha wa timu ya Makilikili fc Jeoseph Lucas amesema wamefikia ushindi huo na kutwa ubingwa wa kata kutokana na  ushirikiano na kujituma wachezaji.
 
Diwani Viti Malumu Kata ya Runzewe Mashariki Mary Nchiba akikabidhi zawadi na Diwani wa Kata ya Runzewe Mashariki Maduhu Mwanambati wamesema katika Kata hiyo zilikuwa zimeshiriki timu 8 lakini Makirikiri Fc imetwaa ubingwa wa Kata hiyo.
Nchiba alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko kwa kudhamini mashindano kila mwaka ili kuibuwa vipaji kwa vijana na kuwajengea Afya.
Makirikiri fc imejinyakulia Zawadi ya ubingwa wa Kata seti moja ya jezi na mpira mmoja huku mshindi wa pili Nampangwe fc walipewa mpira mmoja.

Comments