KILIMAHEWA FC YAICHAPA BUKOMBE UNITED 3-1



Mashindano ya Doto Cup 2019 ngazi ya tarafa yakiendelea kushika kasi timu ya Kilimahewa fc toka kata ya Katente imeichapa goli timu ya Bukombe united toka kata ya Igulwa goli 3-1.
Wafugaji wa timu ya Kilimahewa fc Musa Moja dakika ya 10 Juma Nela dakia ya 25 Mbagara Koster dakikaya 98 huku mfungaji wa goli la timu ya Bukombe United Juma Richard dakia ya 66 kupitia mkwaju wa Penaliti.
   Kwa mjibu wa katibu wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Bukombe (BUFA) Bosco Mwidadi amesema katika Uwanja wa Tarafa ya Bukombe Timu ya Chui FC imeichapa 3-1 Timu ya Iyogelo FC,Uwanja wa Uyovu Timu ya Namonge FC imeibuka na ushidi wa bao 1-0 dhidi ya Namsega FC,na katika Tarafa ya Kisoka Timu ya Sinamila FC imeibuka na Ushidi wa mabao 2-0 dhidi ya Miyenze FC.
Kocha wa timu ya Bukombe United Musa Mzunzu amesema matokeo hayo ameyapokea na kwamba mchezo unamatokeo matatu kushindwa kushinda na sale.
Huku kocha wa timu ya Kilimahewa fc Joseph Kapelo amesema wameshinda kutokana na makosa ya timu ya Bukombe united na kwamba kikosi chake kiko safi atahakikisha ana twa ubigwa wa tarafa.

Comments