FEDHA ZA SERIKALI ZITUMIWE KWA KUEPUKA HOJA ZA UKAGUZI

 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Philibert Nyangahondi akitoa utambulisho wa wageni walioshiriki kwenye Baraza Maalum la CAG liliketi julai18 2019 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo 

  Wataalam wa Idara mbalimbali wakiwa kwenye Baraza Maalum la CAG liliketi julai18 2019 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe

  Madiwani wa Kata mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye Baraza Maalum la CAG liliketi julai18 2019 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Fedha za serikali na michango ya wadau na mapato ya ndani katika halmashauri zinatakiwa kutumika kwa kuepuka hoja za ukaguzi.
Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Robart Gabriel wakati akiedesha kikao cha Maraza maalumu la madiwani kujadili hoja za mkaguzi wa mahesabu ya serikali katika halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.

Gabriel alisema kwa mwaka wa fedha 2017/18 Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe imepata hati safi katika matumizi ya fedha zote.

Gabriel alisema kutokana na hati hiyo safi Halmashauri ilikuwa na hoja 41 za ukaguzi na hoja  6 zimepatiwa majibu sahihi zimebaki hoja 35 za ukaguzi na zinaendelea kupatiwa ufumbuzi wa majibu mazuri.

Aliwataka madiwani na watalamu kushirikiana katika utekelezaji wa agizo la kuepuka hoja za ukaguzi na hati chafu badala yake kwa mwaka wa fedha 2019/20 halmashauri ipate tena hati safi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Safari Mayala alisema kulipo na mafanikio haziwezi kukosa changamoto wamepata hati safi na katika hoja za ukaguzi ni sehemu ya kujifunza na kutekeleza maelekezo ya takayo tolewa na Serikali.

Mayala alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa halmashauri itahakikisha inatekeleza maelekezo ya serikali kwa kufanyakazi katika miradi ya maendeleo kuzingatia kuepuka hoja za ukaguzi.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko aliwaomba madiwani kuhamasisha maendeleo kwa wananchi hasa ujezi wa Zahanati na Vituo vya Afya ili serikali ilete fedha za ukamilishaji itakayo wafanya wananchi kupata huduma karibu.

Comments