DIWANI AWAOMBA WANANCHI KUSHIRIKI KWENYE MRADI WA ZAHANATI

   Diwani wa Kata ya Bulangwa Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita, Yusuph Mohamed amewaomba Wananchi wa Kata hiyo kushiriki kwenye miradi ya maendeleo kwa kujitolea kuchimba msingi na kusongeza mawe, mchanga, na kusomba maji ya kujengea.
Mohamed alitowa wito huo wakati akiwashukru wananchi kuja kujitolea kuchimba msingi wa mradi wa ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Bulangwa.

Alisema katika nguvu za wananchi Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko amechagia sh milioni 6  kwa ajili ya kununua mifuko  250 ya simenti na kusomba mchanga na mawe.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Bulangwa Amos Manumbu amesema mwaka 1999 Kijiji kiliazishwa wananchi na tangu kipindi hicho wamekuwa wakifuata huduma za Afya katika Kituo cha Ushirombo.
Manumbu alisema kutokuwa na Zahanati kijijini hapo ni changamoto kubwa kwa wananchi hasa wanawake wenye ujauzito hali ambayo inayowafanya wengine kutohuzuria kliniki ya mama baba na mtoto.

 Mkazi wa kijiji cha Bulangwa Bundala Migayo aliomba serikali iwaunge mkono wananchi ili waondokane na changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya Afya. 

 Kaimu Mhandisi wa Ujenzi Wilaya ya Bukombe Dominico Shilingo  alisema ujenzi wa Zahanati ya Bulangwa itakamilika kwa mjibu wa mkataba siku 90 hadi kukamilika na itaghalimu Tsh milioni 68 .
 



Comments