Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani
Geita Mhe. Doto Mashaka Biteko amekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh milioni 56 katika Hospitali ya Wilaya ya Bukombe.
Miongoni mwa vifaa tiba hivyo ni vitanda kwa
ajili ya upasuaji na vingine wodini na baiskeli za wagonjwa na fimbo za kutembelea
wazee.
Biteko ambae pia ni Waziri wa Madini
aliushukuru uongozi wa Shdepha+ Kahama kwa msaada wao ikiwa ugonjwa wa kifua
kikuu ni mbaya na pia serikali inabeba mzingo mkubwa wa kutoa matibabu bure.
Waziri wa Madini Biteko alitoa wito
kwa Watanzania wote wanaojishughulisha
na uchimbaji madini kuchukua tahadhali ya kujikinga na maabukidhi ya kifua
kikuu.
Mkurugenzi wa miradi ya Shdepha+
Kahama Venancy Kabwebwe akikabidhi msaada wa piki piki na bajaji alisema kuunga
mkono serikali ilivyo boresha sekta ya afya kwa kujenga zahanati na kuongeza
bajeti kitaifa shdepa imetowa msada wa na Bajaji zenye thamani ya sh 240
milioni.
Kabwebwe alisema katika Mkoa wa Geita Wilaya ya Bukombe
imepewa kipaumbele kutokana na wilaya hiyo imeathilika sana na ugonjwa wa kifua
kikuu.
Alisema Wilaya imeathilika hasa maeneo
ya migodini na vijiji ambako huduma za upimaji hazitolewi vizuri pikipiki hizo na bajaji zitakusanya
makohozi nyumba kwa nyumba na migodini na kukimbiza kwenye maabara ya hospitali
ya Wilaya na kurudisha majibu ili kutoa matibabu kwa wagonjwa.
Mratibu wa ugonjwa wa kifua kikuu Wilaya
ya Bukombe Dk Joshua Mazingo alisema Wilaya ya Bukombe kimkoa inaongoza kuwa na
wagonjwa wengi wa kifua kikuu.
"Vifaa hivi vitasaidia
kuboresha huduma za afya na kuhakikisha wanakusanya makohozi ya watu
wanapopimwa katika vituo vya afya na zahanati kwa wakati" Alisema Mazingo.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Katibu wa Hosptali ya wilaya amesema wamepokea msaada wa pikipiki tano,Bajaji mbili toka shirika la Shdepha+ Kahama kwa ajili ya kitengo cha Kifua kikuu sanjari na vifaa tiba ambavyo ni vitandakwa ajili ya upasuaji ,baiskeli za wagojwa na fimbo za kutembelea wazee kutoka kwa Mbunge Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba aliwataka waunguzi na madaktari
kutunza vifaa vilivyo letwa na wadau wa maendeleo akiwemo mbunge ili visaidie
wananchi.
Comments
Post a Comment