Walimu wa Wilaya ya Bukombe kunufaika na sacos yao


 Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Anjela Kairuki akizungumza na walimu wa Wilaya ya Bukombe katika hafla iliyoandaliwa na walimu hao iitwayo usiku wa mwalimu

 
 Mbunge wa jimbo la Bukombe na Waziri wa madini Doto Biteko akizungumza na walimu wa Wilaya ya Bukombe katika hafla iliyoandaliwa na walimu hao iitwayo usiku wa mwalimu

 
 Mkuu wa wilaya ya Bukombe Said Nkumba akizungumza na walimu wa Wilaya ya Bukombe katika hafla iliyoandaliwa na walimu hao iitwayo usiku wa mwalimu
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe Nikasi Mayala akizungumza na walimu wa Wilaya ya Bukombe katika hafla iliyoandaliwa na walimu hao iitwayo usiku wa mwalimu
Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Bukombe Dionis Myinga
 akizungumza na walimu wa Wilaya ya Bukombe katika hafla iliyoandaliwa na walimu hao iitwayo usiku wa mwalimu  
 
 Mwalimu akisoma risala kwa mgeni rasmi




 
 

 Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Anjela Kairuki akikabidhi zawadi kwa mmoja kati ya walimu wa Wilaya ya Bukombe waliofanya vizuri katika ufaulishaji.
 
 
Walimu wakiwa kwenye umakini mkubwa katika hafla yao

 



 Walimu wakipata burudani ya mziki kwenye sherehe ya Usiku wa mwalimu

Walimu wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, wametaja changamoto
zinazo athiri jitihada za mafanikio ya walimu kukosa chombo cha
kuwaunganisha na kuwainua kiuchumi kama vile Sacos.
Changamoto hiyo ilitolewa na mwalimu Eliya John na Savera Mugisha
wakati wakisoma Risala ya walimu kwenye sherehe yao Juni 8 mwaka 2019
katika ukumbi wa Makuti mjini Ushirombo sherehe walioiita usiku wa
mwalim.

John alisema kutokuwepo chombo cha kuwaunganisha walimu wengi Wilayani
hapa wamekuwa na madeni makubwa na riba kubwa kwenye taasisi za kifedha
lakini kama watakuwa na Sacos itawasaidia kuwa na mikopo nafuu.
Ofisa Elimu kata ya Katente Rehema Makalanga alisema walimu wanatamani
kuwa na sacos ili  walimu kuwana hadhi na kuondokana na vitendo vya
walimu kuzallisha na kuzalilishwa.

Makalanga alisema walimu wamekuwa wakidhalilishwa na wamiliki wa tasisi
za kifedha kwa kunyan’ganywa kadi ya benk mwali anapoenda kuchukuwa
msharaha wake mpaka akapige magoti.

Alisema walimu wakiwa na sacos yao itawaodolea changamoto kukopa
sehemu nyingi sacos ya walimu itawasaidia kukopa kwa heshima na
itawasaidia kujikwamua kiuchumi kwa kuwa na miradi itakayo simamiwa na
walimu.

Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Geita CWT John Kafimbi alisema
walimu wamekuwa wakinyanyasika wanapokopa na kwamba kutokana na
malengo ya walimu wa Bukombe chama kitatowa TSh milioni 1 ya kuanzishia
Sacos.

Nae Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko wakati akiwapongeza walimu
katika sherehe hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi  alisema
atawachangia Tsh milioni 5 walimu ili waendeshe Sacos yao na kujiinua
kiuchumi kwa kufanya biashara ya uzalishaji mali badala ya kutegemea
mshahara peke yake.

Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Anjela Kairuki ambae
alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya usiku wa mwalimu aliwahamasisha
walimu kuunda Sacos ambayo itawaunganisha katika maswala mbali mbali
ya kiuchumi.

Kairuki  alisema bila kufanya hivyo walimu wataendelea kuwa na changamoto za kiuchumi na kubainisha kuwa kuna wengine wanajiweza kiuchumi wameweza kuifikia Benki ya walimu na
Benki mbali mbali lakini kama watakuwa na chombo cha kuwaunganisha
itawasaidia kujiwekea sheria nafuu za kukopa ili kujikwamua kiuchumi.

Comments