Choo cha maturubai cha wachimbaji.
Akina mama wakitafuta mawe ya dhahabu
Zaidi ya wachimbaji wadogo wa madini ya
dhahabu 10,000 katika mgodi usiyo rasmi ulipo katika kijiji cha kakola
namba tisa katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani
Shinyanga wako hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na
kujisaindia vichakani.
Hayo yamebainishwa jana na Mwenyekiti wa kijiji hicho Emmanuel
Nkenze wakati akizungumza na
Waandishi wa Habari waliotembelea mgodi huo, na kusema kuwa tatizo hilo
linahidaji kupatiwa ufumbuzi wa haraka ili kuzuia kuzuka kwa magonjwa ya
mlipuko.
Amesema kuwa vyoo vilivyopo kwa sasa ni
madundu kumi ambayo yanaonekana ni machache ukilinganisha na idaidi ya
wachimbaji wadogo waliopo ambao wanazidi kuongezeka na kila siku hali
huku kasi ya uchimbaji wa vyoo ikiwa ni ndogo huku wengi wao hawatambui
umuhimu wa kujisaidia katika maeneo salama.
Baadhi ya wachimbali katika Mgodi huo akiwemo Samwel
Joseph na Esta Shija wamesema kwa
sasa hali sio nzuri katika eneo hilo kwani wachimbaji wengi hawana
desturi ya kujisaidia katika vyoo na kuziomba mamlaka husika kulipatia
ufumbuzi wa haraka ili kuzuia watu kupata magonjwa kwani idadi ya
wachimbaji inazidi kuongezeka.
Wamefafanua kuwa gharama za kujisaidia
katika vyoo vilivyopo katika eneo hilo ni kubwa jambo ambalo wao
wameshindwa kuimudi kwani zinabadilika badilika mara kwa mara katika
vyoo vilivyopo katika maeneo hayo na kusababisha wengi wao kwenda
kujisaidia vichakani.
Naye Msimamizi mkuu wa Mgodi huo Husein
Makubi Ngh’wananyazala amekiri
kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa kwa sasa ofisi yake imewekeza
nguvu kubwa katika ujenzi wa vyoo ili kukabiliana na Tatizo la uhaba wa
matundu ya vyoo ikilinganishwa na idadi kubwa ta wachimbaji.
Hata hivyo amesema kuwa, tatizo la
upungufu wa vyoo mgodini umetokana na uongezeko la wachimbaji wadogo
ambao wamekuwa wakiongezeka kila siku kutokana na eneo hilo kuwa na
wingi wa madini.
Amesema kuwa, ili kuendelea kupamaba na
uhaba huo wameanza kuwahamasisha wamilikiwa wa nyumba za kulala wageni
zilizojengwa katika eneo hilo,kuhakikisha wanajenga vyoo kabla ya
kufungua nyumba yake ali ambayo itapunguza adha ya wachimbaji kujisaidia
vichakani.
Akiongea kwa niaba ya wachimbaji wadogo
Samweli Joseph alisema kuwa, sababu inayopolekea wachimbaji wadogo
kujisadia vichakani,inatokana na gharama ya shilingi 3,00 za kujisaidia
katika vyoo viliyopo na kufanya wengi wetu kujisaidia vichakani
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi
Macha amesema kuwa ujenzi wa vyoo katika Mgodi huo unandelea kujengwa kwa haraka ili kuhakikisha Tatizo hilo linakomeshwa mara mmoja.
Comments
Post a Comment