Das Cheyo awashukia watumishi wa Bukombe


 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe  Paul Cheyo akimkabidhi hati ya majengo  Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Kituo cha Afya Ushirombo Antony Kuya tayari kwa kuanza kutumika.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe  Paul Cheyo wakiwa na viongozi mbalimbali wakijiridhisha  moja ya vifaa tiba vilivyowekwa kwenye Mjengo hayo mapya.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Dioniz Myinga akizungumza wa watumishi katika makabidhiano hayo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe  Paul Cheyo wakiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya majengo hayo.


 



Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita, Paul Cheyo
amewataka watumishi wa Umma kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya
utumishi wa umma na kuto omba rushwa.

Cheyo alitowa wito huo wakati akihutibia watumishi wa umma na
kukabidhi mradi wa majengo ya huduma mbali mbali za  afya katika kituo
cha Afya Ushirombo Kata ya Bulangwa kwa niamba ya Mkuu wa Wilaya ya
Bukombe Said Nkumba kwa watalamu ili yaanze kutumika kuhudumia
wananchi.

Cheyo alisema majengo yamejengwa lengo la serikali ni kuboresha huduma
za Afya kwa wananchi.

Aliwataka madaktari na waunguzi kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa
wagonjwa na kujiepusha na vitendo vya rushwa badala yake watoe lugha
nzuri kwa wagonjwa.

Alisema iwapo watalamu wa Afya katika kituo hicho watatoa huduma
vizuri kwa wagonjwa kwa kuzingatia madili itapunguza msongamano wa
wagonjwa kwenye Hospitali ya Wilaya.

Cheyo alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Dioniz Myinga kufatilia vifaa tiba

hasa vya chumba cha Upasuaji na kuhakikisha anaongeza madaktari na
waunguzi wa kutosha katika kituo hicho cha afya ili kuondoa changamoto
ya utoaji huduma kwa wagonjwa kwa wakati.

Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi kituo cha Afya Ushirombo Antony Kuya
alisema wamejenga jengo la wazazi, jengo la upasuaji, Nyumba ya
maabara ya kisasa, nyumba ya mtumishi moja, Nyumba ya kuhifadhi maiti,
 jengo la kufulia nguo,  barabara ya kutembelea wagonjwa, jengo la
kupokea na kusambaza umeme.

Kuya alisema mradi huo serikali ilileta fedha sh 500 milioni kati ya
fedha hizo zilizotumika hadi kukamilika sh 461.4 milioni na kubaki
chenchi sh 1.8 milioni.

Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Ushirombo Dk Henry Sahani alisema ujenzi
ulianza Julai mwaka 2018 na umekamilika Februari 2019 kituo hicho cha
afya ni miongoni mwa vituo nchini vilivyopata fedha toka serikali
kupitia mfuko wa Afya.

Dk Sahani alisema  kabla hawaja kamilisha jengo la upasuaji kulikuwa
na changamoto kubwa tangu januari mwaka 2019 wagonjwa waliopewa rufaa
kwenda Hospitali ya Wilaya kufanyiwa upasuaji 40 hasa kina mama
wanaoshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.

Dk Sahani alisema kituo cha Afya Ushirombo kinapokea wagonjwa kutoka
Kata jirani ya Lyambangongo, Ushirombo na ya Igulwa serikali itakapo
leta vifaa chumba cha upasuaji inatakiwa serikali pia kuongeza
watalamu ili huduma iwe bora zaidi kwa wananchi.

Comments