
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda
kuwatangazia wananchi wote kuwa, itashiriki Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma kuanzia tarehe 17 hadi 22 Juni 2019. Maadhimisho haya
ni kwa mujibu wa kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama
huadhimisha kwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu Utumishi wa
Umma.
Wakati wa maadhimisho hayo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki imeandaa madawati maalum ya kutoa huduma kwa wananchi
katika Ofisi za Wizara zilizopo Kata ya Mtumba jijini Dodoma na zile
zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Huduma zitakazotolewa ni pamoja na kusikiliza na kutoa ufafafanuzi wa
hoja mbalimbali za wananchi kuhusu Wizara pamoja na kutoa elimu kuhusu
majukumu yanayotekelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika.
Madawati hayo yatakuwa wazi kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.
NYOTE MNAKARIBISHWA.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
Comments
Post a Comment