Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akizungumza Katika kikao cha Baraza la Madiwani Wilayani Bukombe
Bukombe,Serikali imetoa masaa 84
kwenye makampuni manne yaliyofunga mkataba wa kununua zao la pamba wilayani Bukombe
mkoani Geita wawe wameanza kununua pamba hiyo.
Tamko hilo la serikali lilitolewa na
mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Said Nkumba saa 9:58 alasili juni 20
mwaka huu kwenye kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bukombe.
Nkumba alimuagiza mkaguzi wa pamba
wilaya ya Bukombe Edmond Jemes kuhakikisha itakapo fika saa 8:00 mchana Juni 24
kama kutakuwa na kampuni ya kununua pamba halija fika kwenye kituo apate
taarifa ili achukuwe hatua.
Alisema kwenye taarifa za madiwani Juni
19 wakati wakiwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuri za maendeleo na
changamoto za wakulima walidai baadhi ya wakulima wameaza kutorosha zao hilo na
kwenda kuuzia wilaya jirani na halmashauri inakosa mapato.
Bazi ya makampuni matatu mameneja
walifika kujibu na kutoa sababu zilizo chelewesha kunaza kununu pamba Furesho,
KCCL na Kahama oil mili, huku inadaiwa kuna makampuni manne yaliyofunga mkataba
kununu pamba wilaya ya Bukombe yote matawi ya Kahama.
Meneja wa kampuni Furesho Kifashizi
Ngalula akiwa kwenye baraza alisema bei ya sh 1200 ilikuwa inawakata na kampuni
inatalajia kufungua vituo vya kununuria pamba jumatatu kilichowasababisha
kuchelewa kuanza ununuzi ni kutokana na kushuka kwa bei ya pamba soko la
duniaanaishukuru serikali imesha kaa na wadau na wamekubaliana kuanza kununua
pamba.
Meneja wa kampuni ya KCCL Edward
Lubacha akijitetea kwenye baraza alisema
tangu Mei 2 walisuwa suwa kuanza kununu kwa
kupolomoka kwa bei ya kidunia na kwamba kampuni linatalajia kuwa na
vituo 46 za kununulia pamba wilayani Bukombe.
Meneja wa kampuni ya Kahama oil mili Amos Ndutu aliliambia baraza
la madiwani kuwa jumatatu kampuni ita anza kununua imeingia na mkataba na vyama
vya msingi 47 walichelewa kuanza kutokana na
kushuka kwa bei ya soko la pamba kidunia lakini kwa sasa serikali
imefikia muafaka na wakurugenzi wa makampuni.
Upandewake mkaguzi wa pamba wilaya ya
Bukombe Edmond Jemes akipokea maelekezo ya serikali yaliyotolewa na mkuu wa
wilaya hiyo aliwahakikishia madiwani kuwa makampuni yameelekezwa kuto shusha
bei ya sh 1200 kwa kilo moja.
Jemes alisema nikweli kwamba bei ya
pamba kidunia ilikuwa imeshuka hadi kufikia sent paund 75 na imeendelea
kupolomoka hadi sasa ni senti 67 sawa na sh 1060 ya kitanzania na Mei 1 msimamo
wa serikali ilikuwa makampuni wanunuwe kwa sh 1200 kwa kilo na hata sasa
serikali imeelekeza waingie sokoni kwa bei ya sh 1200 kwa kilo na hakuna kukopa
pamba kwa wakulima.
Mwenyekiti
wa halmashauri Safari Mayala alisema kwa maangizo ya mkuu wa wilaya kama
halmashauri watayafanyia kazi na kampuni ambayo itakuwa haija ingia sokoni
kununua pamba serikali ya wilaya ya Bukombe itafuta mkataba na kampuni ambalo
halita tekeleza angizo la serikali ili halmashauri itafute makampuni mengine
ispoteze mapato.
Comments
Post a Comment