Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akizungumza na vijana waliohudhuria semina ya kitalu nyumba Wilayani Bukombe
Serikali imewaka vijana
kuwanaushirikiano wanapokuwa wanafanya shughuli za uzalishaji wa mali kwa lengo
la kujikwamua na umaskini.
Wito huo ulitolewa na mkuu wa wilaya
ya Bukombe Said Nkumba wakati akifungua mafunzo ya siku nane vijana 100 mafunzo
yanayolenga kuhudumia mazo ya bustani kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba
kata ya Bulangwa wilaya ya Bukombe mkoa
wa Geita.
Nkumba alisema serikali imetowa sh 13
milioni toka ofisi ya waziri mkuu kwa vijana wilaya ya Bukombe ili wanufaike na
kilimo cha kitalu nyumba.
Aliwataka vijana baada ya mafunzo
haya wawe na hamasa ya kuendelea kulima kiliomo chakitalu nyumba kwa kuzingatia
mafunzo na teknolojia wanayopewa.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
wilaya ya Bukombe Dioniz Myinga aliwaomba vijana ambao wamekuja kujifunza
mafunzo hayo kuwa chachu ya maendele kwenye vijiji ili mradi huu ufike kila
kijiji.
Myinga alisema kilimo cha kitalu
nyumba kitawapa ajila ya kujiajiri vijana na kukuza uchumi kuanzia ngazi ya
familia na taifa.
Mtalamu wa kuchanganya udongo na
upandaji mazao ya bustani kwa kutumia teknolojia Joseph Athanas toka kampuni ya
Holygrnee agric limited iliyopo mkoani Morogoro (vijana sua) ambaye pia
muwezeshaji wa mafunzo hayo.
Athanas alisema kampuni hii imepewa
tenda na serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu kutowa mafunzo kwa vijana 100
kila wilaya hapa nchini kwa kushirikisha vijana wa malika yote hadi umri wa
miaka 36 awe amesoma hata kama hajasoma.
Athanas aliongeza kuwa serikali kwa
kupitia mafunzo hayo vijana wengi watanufaika badara ya kupitia vikundi vya
vijaja na walemavu na wanawake kwa kusubili mkopo wa halmashauri.
Mafunzo haya yatawafanya vijana
kujitegemea wao kuendeleza kilomo badara ya kutegemea fedha za halmashauri
kupitia mapato ya ndani asilimi 4 ya vijana asilimia 4 ya wanawake asilimia 2
walemavu hali ambayo zimekuwa haziwanufaishi.
Rahery Ernest ambae nimshiriki wa
mafunzo alisema wanaishukru serikali kwa kuwaletea mafunzo kupitia mafunzo haya
wataenda kuazisha kilimo cha kitalunyuba vijiji ili kuhakikisha vijana
wanajikwamua kiuchumi.
Comments
Post a Comment