
Rais Magufuli amesema kuwa anatamani wakati atakapomaliza muda wake wa uongozi, Tanzania iwe na mabilionea zaidi ya 100.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo katika Ikulu ya Dar es Salaam wakati
akizungumza kwenye mkutano kati yake na wafanyabiashara kutoka wilaya
zote za Tanzania kwa lengo la kujadili changamoto zinazokwamisha sekta
hiyo.
Magufuli
amesema jambo hilo litamfanya afurahi kuona anamaliza muda wake huku
akiacha mabilionea wengi nchini kutokana na kile alichokuwa akikifanya
katika kuboresha mazingira ya biashara.
“Thubutuni
na msiogope kufanya biashara ya aina yoyote, nchi yetu imebarikiwa kuwa
na ardhi nzuri, rutuba, maji kwa ajili ya uvuvi, mifugo, madini fursa
nyingi za uwekezaji zitumieni ili ziwanufaishe ili siku nikiwa naondoka
angalau niache wafanyabiashara mabilionea zaidi ya 100, nitafurahi
sana.” Amesema.
Rais Magufuli pia ameashiria changamoto za biashara katika mipaka ya
nchi hiyo na amewataka wafanyabiashara hao kutumia fursa ya masoko ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini
mwa Afrika (SADC)
Comments
Post a Comment