Mahakama
Kuu ya Tanzania imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa mlinzi wa
shule ya Scolastica mkoani Kilimanjaro, Hamis Chacha kwa kosa la kumuua
aliyekuwa mwanafunzi wa shule hiyo, Humprey Makundi.
Pia, Mahakama hiyo imemuhukumu mmiliki wa shule hiyo, Edward Shayo na
aliyekuwa mwalimu wa nidhamu, Labani Nabiswa kifungo cha miaka minne
jela kila mmoja wa kosa la kuficha ukweli wa mauaji ya mwanafunzi huyo.
Hukumu hiyo imetoelewa leo Jumatatu Juni 3, 2019 na Jaji Firmin Matogolo
baada ya kumtia hatiani Chacha kwa kumuua kwa makusudi mwanafunzi huyo
wa kidato cha pili, Makundi.
Mwanafunzi huyo aliuawa Novemba 6,2017 na baadaye mwili wake kutupwa mto
Ghona, mita takribani 300 kutoka shuleni na baadae kuzikwa na Manispaa
kabla ya kufukuliwa kwa amri ya mahakama.
Comments
Post a Comment