BITEKO AWAOMBA WADAU WA MICHEZO KUWASHIKA MKONO WANAFUNZI WALIOFAULU KWENDA KUSHIRIKI MASHINDANO YA UMITASHUMITA MKOA




Mbunge wa Bukombe Doto Mashaka Biteko akisalimiana na walimu waliojiandaa kushiriki mechi ya netiboli


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko aliwaomba walimu wanaokwenda na wanamichezo kuwatunza na kuwajengea uwezo wanafunzi hao ili wafanye vizuri ikiwezekana kuwa wa kwanza kwa mkoa wa Geita.
Mkuu wa  Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akikabidhi zawadi kwa mshindi
Biteko aliyasema hayo katika viwanja vya shule ya Ushirombo sekondari wakati akikabidhi sh milioni 1 kwa ajili ya kuwasaidia wanamichezo wa umitashumita.
Walimu wakishiriki shindano la kufukuza kuku kwenye Bonanza la siku ya Mwalimu katika wilaya ya Bukombe

Kwa upande Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Saidi Nkumba amewaomba wafanyabiashara na wadau wa michezo Wilayani hapa kuwachangia fedha na vifaa vya michezo ili wakafanye vizuri kwenye mashindano ya umitashumita ki mkoa.




Wito huo aliutowa wakati akiwaaga na kukabidhi Bendera ya halmashauri ya Bukombe wanafunzi 100 toka shule tofauti tofauti za msingi wilayani hapa waliofaulu kuingia kwenye umitashumita kimkoa kwa michenzo mbali mbali .

Nkumba alisema halmashauri ya Wilaya ya Bukombe imewezesha na baadhi ya wadau wa michezo wamewezesha vifaa na kwamba katika sherehe hizo Mkuu wa Wilaya aliwakabidhi vifaa vya michezo vipya mipira minne yenye thamani ya sh 400,000.
Meneja wa Umitashumita Mwalimu Joseph Kabote alishukuru sana misaada ya waadau akiwemo Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko kwa kuwapa fedha akiwa ni mdau mkubwa wa michezo kwa Wilaya ya Bukombe
Kabote aliongeza kuwa mchango wa Mbunge huyo utawasaidia kununua vifaa vya michezo kwa wanafunzi na watanufaika na viongoziwao wa serikali.
Na kuwaomba wadau kuendelea kuwachangia ili wanamichezo wakafanye mashindano bila hofu ya aina yeyote ili  watafanye vizuri.

Comments