Waziri wa Madini, Doto Biteko (pichani) amefanya uzinduzi wa Soko Kuu la
Madini Mwanza na kutumia fursa hiyo kuwahimiza wachimbaji na
wafanyabiashara wa madini kutumia soko hilo kuuzia madini yao na
kuachana na tabia ya utoroshaji wa madini.
Uzinduzi wa soko hilo unganishi Kanda ya Ziwa umefanyika leo Mei 08,
2019 katika jengo la Rock City Mall ambapo Biteko amebainisha kwamba
uanzishwaji wa masoko ya madini nchini umesaidia ongezeko la kiwango cha
uuzaji madini tofauti na hapo awali ambapo yalikuwa yakiuzwa kiholela
na hivyo kuikosesha Serikali mapato.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akitoa salamu za tume kwenye uzinduzi huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akitoa taarifa ya
hali ya uanzishwaji masoko ya madini nchini ambapo amebainisha kwamba
zaidi ya mikoa 10 tayari imeanzisha masoko hayo.
Mfanyabiashara wa madini, Kakono Kaniki akitoa salamu kwa niaba ya wafanyabiashara wa madini mkoani Mwanza.
Comments
Post a Comment