
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Rai
hiyo imetolewa Mei 14,2019 jijini Dodoma na Naibu katibu mkuu
Utumishi, Bw.Francis Michael katika ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Mwaka
wa Baraza la wafanyakazi wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi hesabu za Serikali
C.A.G.
Bw.Michael
amesema kuna baadhi ya watumishi wa Umma wamekuwa wakikiuka maadili ya
kazi na taaluma zao na kujikita wakiwa watovu wa nidhamu na kujikita
kwenye masuala ambayo yako kinyume na utaratibu wa kazi hivyo ni vyema
kwa kila mfanyakazi akazingatia maadili ya kazi zake.
Hata
hivyo,Bw.Francis ameipongeza ofisi ya ukaguzi wa hesabu za serikali
,C.A.G ikiongozwa na kiongozi wake Mahiri Profesa Musa Assad kwa
kuendelea kutoa ripoti ya ukaguzi kwa wakati kila mwaka bila upendeleo
wowote katika kusukuma gurudumu la Maendeleo kwa kuelekea Uchumi wa
kati wa Tanzania ya viwanda.
Kuhusu
changamoto zinazoikabili ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za serikali C.A.G
hususan upungufu wa wafanyakazi Bw.Francis amesema ofisi yake ipo tayari
kutatua tatizo hilo ambapo ameitaka ofisi ya C.A.G kufanya mchakato wa
kuorodhesha idadi husika ya upungufu huo.
Katibu
wa TUGHE Taifa Heri Mkunda amezungumzia juu ya Ushirikishwaji wa
wafanyakazi katika bajeti ili kujenga dhana ya utawala bora .
Kwa
upande wake mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ofisi ya Taifa ya
ukaguzi C.A.G Prof.Musa Assad amesema ofisi yake ina watumishi 957
huku kukiwa na upungufu wa watumishi zaidi ya hamsini kutokana na
sababu mbalimbali ikiwemo kustaafu,kufariki au kuhamishwa taasisi
nyingine.
Kaulimbiu ya mkutano mkuu wa mwaka wa Baraza la Wafanyakazi ya ofisi
ya Taifa ya Ukaguzi ni Ukaguzi Shirikishi ,Uwazi na Uwajibikaji ni nguzo
muhimu katika kufikia uchumi wa kati
Comments
Post a Comment