
Serikali
imesema itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria wamiliki wa
Bar kote nchini wanaopiga muziki mkubwa katika bar zilizokaribu na
Makazi ya watu na kusababisha kero kwa Wakazi husika na kukosa usingizi.
Rai
hiyo imetolewa leo Mei 22,2019 na Waziri wa Ofisi ya Rais[TAMISIMI]Mhe
Seleman Jafo wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Maryam Salum
Msabaha aliyehoji ,kuna baadhi ya Bar na Club ambazo zimejengwa kwenye
makazi ya watu ambazo zimekuwa na kero kwa jamii kwa kupiga muziki
mkubwa na usiozingatia Maadili ya Kitanzania, je,nini kauli ya Serikali
kuhusu Bar na Club ambazo zinakiuka maadili ya jamii na sheria.
Katika
majibu yake ,Waziri wa Ofisi ya Rais ,TAMISEMI Mhe.Seleman Jafo amesema
serikali inawaelekeza wamiliki wote wa Bar na Club kuzingatia maelekezo
ya sheria ya Vileo Na.28 ya Mwaka 1968 kifungu cha 14[1] katika
uendeshaji wa shughuli zao ambapo amesema serikali haitasita kuchukua
hatua kwa vitendo vyovyote vitakavyobainika kukiuka sheria na
kusababisha kero kwa wananchi wengine.
Kutokana
na Bar na Club kuwa kero katika makazi ya Watu kwa kupiga muziki
mkubwa ,Waziri Jafo amewaagiza viongozi wa Serikali za mitaa wakiwemo
wakuu wa wilaya na Mikoa kote nchini kufuatilia jambo hilo .
Naye
Mbunge wa Rombo,Joseph Selasini amehoji,Mara nyingi Bar zimekuwa
zikijengwa kwa kutozingatia mipango miji na watu wenye Madaraka
wakiwemo wabunge wenyewe kwanini Serikali isitoe tamko juu ya Bar
zinazojengwa Ovyo ovyo iwe Marufuku na mtu atakayetoa kibali cha ujenzi
akamatwe.
Akijibu
swali hilo,Waziri Seleman Jafo amesema sheria zipo na kinachotakiwa ni
kusimamia sheria husika kwa viongozi wa serikali za mitaa na kufanya
ufuatiliaji dhidi ya wamiliki wa Kumbi za starehe wanaokiuka sheria
hizo.
Comments
Post a Comment