VIONGOZI WA SERIKALI WAAGIZWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUTUNZA VYANZO VYA MAJI


Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba Mwenge wa Uhuru 2019 katika eneo la Namparahara Kata ya Busonzo.
 
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akikiri kupokea Mwenge wa Uhuru 2019

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2019 Mzee Ali akitoa neno la shukrani kwa Wilaya ya Chato

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2019 Mzee Ali akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko.


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akiwa ameshika mwenge wa uhuru 2019.


Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru 2019.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2019 Mzee Ali akitoa Ujumbe wa Mwenge katika viwanja vya Namparahara Wilayani Bukombe.



Mmoja wa viongoji wa Dini akitoa dua kwenye mapokezi ya mwenge wa uhuru mwaka 2019.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na Wakazi wa Naparahara kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2019


Wananchi wakiwa kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2019

Shamrashamra za mwenge wa Uhuru 2019 njiani.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2019 Mzee Ali akifanya zoezi la upandaji miti-Ikuzi Wilayani Bukombe





Wananchi Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, wameagizwa kutunza vyanzo vya maji kwa kutunza misitu na kupanda miti badala ya kufyeka miti au kufanyia shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji.

Agizo hilo lilitolewa kwa viongozi wa serikali kusimamia kutunza vyanzo vya maji kwa kushirikiana na wananchi na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2019 Mzee Ali wakati akishiriki kupanda miti katika mradi wa upandaji miti na kutunza wa mazingira katika kijiji cha Ikuzi kata ya Runzewe mashariki.

Ali alisema maji ni rasilimali muhimu sana kwa matumzi ya mwanadamu kwa kulitambuwa hilo kupitia ilani ya Uchanguzi ya 2015 hadi 2020 inachukuwa hatua mbalimbali kuhakikisha  wananchi wanao ishi vijiji ifikapo 2020 wanapata maji safi na sala kwa asilimia 85 na wanaoishi mjini serikali itahakikisha wanaendelea kunufaika.

Alisema serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya Zanzibar imefunga mkataba na serikali ya India kupewa sh milioni 500  za kimarekani ili wananchi wa bara na visiwani wanapata maji safi na salama.

Afisa Mazingira Wilaya ya Bukombe Francis Innocent akisoma taarifa ya mradi huo alisema mradi huu wa upandaji miti ni kielelezo cha upandaji miti na uhifadhi wa mazingira mpaka sasa miti 241,021 imesha pandwa.

Innocent alisema hamasa imeendelea kutolewa kwa kila shule  na kaya ili kutunza maeneo ya miti ya asili na kupanda maeneo yaliyo wazi kutokana na utunzaji wa mazingira sememu kubwa ya Wilaya imezungukwa na miti na kuifanya Wilaya ya Bukombe kuwa ya kijani.

Alisema Wilaya inahifadhi za misitu tano na pori moja la akiba na kuifanya Wilaya zaidi ya asilimi 75 ya eneo kuwa la hifadhi na kwamba mradi wa upandaji miti Ikuzi ulianza Aprili 1 mwaka huu na kukamilika Aprili 30 mwaka huu kwa kupanda miti 4,000  kati ya hiyo miti 3,800 ni yambao miti 200 ya matunda katika eneo la ukubwa wa hekta 1.5 na mradi umegharimu sh 1.4 milioni.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akipokea mwenge katika kijiji cha Nampalahala Kata ya Busonzo ukitokea Wilaya ya Chato alisema mwenge wa uhuru ukiwa Wilaya ya Bukombe utakimbizwa kilomita 121 na kupitia miradi 12 kati ya miradi hiyo 4 itawekewa jiwe la msingi  miradi 3 itazinduliwa miradi 5 itaonwa au kutembelewa miradi yote inathamani ya sh bilioni 1.340. 
 




Comments