SERIKALI YAAGIZA SHUGHULI ZA MGODI WA IKUZI KUSIMAMIWA NA HALMASHAURI YA BUKOMBE

Naibu Waziri wa Madini  Stanslaus Nyongo akizungumza na wachimbaji wadogo wadogo wa mgodi wa ikuzi Wilayani Bukombe



Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akimhakikishia naibu waziri wa madini kutekeleza maagizo ya serikali aliyotoa kwa wanaushirika.



 Serikali imeagiza shughuri za uendeshaji wa mgodi uliokuwa unasimamiwa na wanaushirika Kijiji cha Ikuzi Kata ya Runzewe Mashariki Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita kuanza kusimamiwa na halamshauri ya Wilaya ya Bukombe hadi watakapo maliza migogoro yao na kupewa leseni ya uchimbaji.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza na hadhara ya wachimbaji wa Ikuzi na wanaushirika Mei 10 mwaka huu. alisema mgodi huo ulitakiwa kufungwa.

Nyongo alisema mgodi wa Ikuzi kutokana na migogoro iliyopo ya wachimbaji wadodo wadogo kulalamikia kutozwa asilimia 4 wanachama wa ushirika walilalamikia uongozi kuwa hautendi haki mgodi ulitakiwa kufungwa.

Nyongo alimuangiza Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba na Mkurungezi Mtendaji wa Halmshauri Dionis Myinga kusimamia mgodi huo ili  kuhakikisha serikali isipoteze mapato na wachimbaji wadogo wadogo wanufaike kwa kutozwa asilimia ndogo ya tozo.

Kwa  upande wa wanaushirika Shija Ramadhan na Switibert Robart walimshukru Naibu Waziri wa Madini kwa uamuzi huo kwani tangu ushirika uundwe hawajawahi kukaa kikao chochote wala kuhusishwa  juu ya mapato ya mgodi na kujua maslahi ya wanaushirika.

Ramadhani alisema tangu Septemba 2 mwaka 2014 alitowa sh 110,000 ikiwemo hisa ya uwanachama mpaka sasa hawajawahi kusomewa mapato na matumizi wala kugawana kujua hisa yake atakuwa na kiasi gani cha fedha.

Robart alisema mwenyekiti wa ushirika tangu achanguliwe hajaitisha mkutano wa wanachama wa ushirika kujuwa fedha zilizopo inagwa wanao mwenyekiti amekuwa akitiwa fedha za ushirika kwenye miradi ya maendeleo ya kijiji hatujuwi ni fedha za ushirika au ni zake binafisi aliomba  serikali kuendelea kutupia jicho Ikuzi kunafeza za mapato ya ushirika na serikali yako mifukoni kwa watu.  


Katibu wa chama cha ushirika Ikuzi Stanslaus Mkwavi akitoa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za makusanyo ya wanaushirika na kuiomba serikali iwape leseni mbele ya Naibu Waziri wa madini.  


Mkwavi alisema mgodi ulianza mwaka 2017 na ushirika uliweka uongozi mbali mbali kwenye mgodi kupitia makusanyo ushirika umelipa mapato serikali kuu  sh 200. 88 milioni Halmashauri ya wilaya imesha chukuwa sh 150.2 milioni kijiji cha Ikuzi wamelipwa sh 100.2 milioni na chama cha ushirika kimechangia fedha kwenye miradi ya maendeleo  sh 41.5 milioni.  


Naibu Waziri wa Madini Nyongo aliiomba kamati ya ulinzi na  usalama Wilaya kupitia vyombo vyake vya uchunguzi kuchunguza chama hicho cha ushirika ikiwa inaonyesha makusanyo hayo ni ya hivi karibuni kuna mianya ya upotevu wa fedha na akaonge kuwa serikali haiwezi kutoa leseni kwenye ushirika huo hadi watakapo mariza tofauti zao na wachimbaji.
 
Mchimbaji wa dhahabu Juma Rashidi  alisema wanatozwa asilimia  nne  kwa washirika ikiwa hawana hata leseni ya uchimbaji wa madini na kwamba kutokana na hali hiyo inawafanya wachimbaji watoroshe dhahabu na kwamba iwapo wachimbaji watapunguziwa asilimia hakika hakuna utoroshwaji wa dhahabu kabisa.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba alisema atasimamia maelekezo ya serikali na kuhakikisha ushirika unafata tamko la serikali nakwamba wanaushirika wahakikishe wanafanya mkutano wa chama mapema.



Comments