Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanunuzi wa madini aliyefungua soko leo
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab
Telack akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliohudhuria
ufunguzi wa soko la pili la madini katika Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 3
Mei, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiwasili
katika eneo la soko la madini na kupokelewa na viongozi wa Chama cha
wachimba madini Mkoa wa Shinyanga mapema leo tarehe 3 Mei, 2019.
Katibu wa Chama cha Wachimbaji madini
Mkoa wa Shinyanga Bw. Gregory Kibusi akitoa neno katika ufunguzi wa soko
la madini lililopo Wilaya ya Shinyanga leo tarehe 03 Mei, 2019.
Baadhi ya wananchi na wadau wa madini waliohudhuria ufunguzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi Mhe. Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani).
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba madini
Mkoa wa Shinyanga Bw. Hamza Tandiko akizungumza katika tukio hilo mapema
leo tarehe 03 Mei, 2019
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab
Telack amefungua soko la madini leo tarehe 03 Mei, 2019 katika Wilaya ya
Shinyanga likiwa ni soko la pili baada ya soko jingine kufunguliwa
Wilayani Kahama mwezi mmoja uliopita.
Akitoa hotuba ya ufunguzi wa soko hilo
katika eneo la Ofisi ya CCM Mkoa ambapo wafanyabiashara tisa (9) wa
Dhahabu na Almasi wamefungua masoko yao hapo, Mhe. Telack amesema tangu
agizo la Mhe. Dkt. John Magufuli la kufungua masoko ya madini, tayari
madini ya dhahabu yenye gramu 30,924.44 yameshauzwa katika soko la
Kahama yakiwa na thamani ya sh. Bilioni 2.9.
Telack amewashukuru wafanyabiashara hao kwa kuitika wito wa Serikali na kufungua soko katika Mkoa wa Shinyanga.
Aidha, ametoa wito kwa wachimbaji
wadogo, wauzaji na wanunuzi kutumia soko hilo la madini na waache
kuuziana madini sehemu zisizo rasmi na atakayekamatwa anafanya hivyo
madini yatataifishwa na wahusika watashtakiwa kwa mujibu wa sheria.
Kaimu Afisa Madini Mkazi Mhandisi
Giliard Luyoka, akisoma taarifa ya madini Mkoa, amesema hadi sasa Mkoa
una wafanyabiashara wakubwa 9 na wadogo 22 na kuwa licha ya Mkoa kuwa na
utajiri wa madini yenye thamani ambapo wachimbaji wadogo wanazalisha
wastani wa kilo 600 za dhahabu na karati 1300 za almasi kwa mwaka,
hakukuwa na masoko rasmi ya uuzaji wa madini hivyo kupelekea utoroshwaji
wa madini hatimaye Taifa kutonufaika na madini hayo.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Wachimba
madini Mkoa wa Shinyanga Bw.Hamza Tandiko amesema kuwa, wanaunga mkono
juhudi za Serikali katika kuhakikisha madini yote yanayopatikana Mkoani
Shinyanga yanawasaidia wananchi wa Mkoa huu kwa kuchangia pato la Taifa.
Comments
Post a Comment