
Na Paschal Dotto
RAIS
Dkt. John Magufuli ameitaka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutoa kipaumbele katika
uwekezaji wa miundombinu ya mawasiliano kwa Kampuni ya Mawasiliano
Nchini (TTCL) ili liweze kumiliki idadi kubwa ya minara ya mawasiliano
ya simu na kumudu ushindani wa soko la mawasiliano nchini.
Akizungumza
katika hafla ya upokeaji wa Gawio la Serikali la Tsh Bilioni 2.1 kutoka
TTCL, leo Jumanne (Mei 21, 2019), Rais Magufuli alisema njia pekee ya
kuiendeleza TTCL ni kwa Viongozi na Watendaji wa Serikali kuwa na moyo
wa uzalendo wa kusimamia rasilamali za umma ikiwamo za shirika hilo.
Kwa
mujibu wa Rais Magufuli alisema TTCL imekuwa ikitumia kiasi cha Tsh
Milioni 700-800 kila mwezi kwa ajili ya kukodisha minara ya mawasiliano,
wakati Serikali ina mfuko wa mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unaotoa
ruzuku kwa makampuni mbalimbali ya mawasiliano kwa ajili ya kujiwekeza
katika miundombinu ikiwemo minara ya mawasiliano maeneo mbalimbali
nchini.
“Hili
la TTCL kukopa minara katika makampuni mengine halikubaliki, Serikali
ina mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ambao wanatoa ruzuku kwa
makampuni mengine ya simu lazima tulitazame upya, nataka sasa TTCL
tuwape mitaji ya kutosha ili kuhakikisha kuwa linaendelea kupanua huduma
zake kwa Watanzania wengi zaidi” alisema Rais Magufuli.
Aidha
Rais Magufuli aliitaka Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha inaipatia
TTCL kiasi cha Tsh Bilioni 30 kilichobaki kati ya Tsh Bilioni 66
ilizotoa katika mwaka wa fedha 2018/19 kwa ajili ya kupanua mtandao wa
huduma zake nchini, kwa kuwa Shirika hilo limeonesha mafanikio makubwa
zaidi katika kipindi kifupi tangu serikali ichukue uamuzi wa kununua
hisa zake kutoka kampuni ya Airtel mwaka 2016.
Akifafanua
zaidi Rais Magufuli alisema Serikali itandelea kuiwezesha TTCL ili
iweze kupanua mtandao wa mawasiliano yake nchini, na kuhakikisha kuwa
linatekeleza vyema majukumu yake ikiwemo kusimamia mawasiliano ya
Kimkakati nchini kupitia Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa kufuatia
kupitishwa kwa Sera ya Taifa ya TEHAMA mwaka 2016.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema TTCL
imeendelea kupiga hatua kubwa zaidi katika utoaji wa huduma ya
mawasiliano nchini ambapo katika mwaka 2018/19, shirika hilo limeweza
kupata faida ya Tsh Bilioni 8.3 ambapo kiasi cha Tsh Bilioni 2.1 imetoa
gawio kwa Serikali.
“Katika
mwaka 2017/18, tulitoa Tsh Bilioni 1.5, lakini kwa mwaka huu tumetoa
Tsh Bilioni 2.1 ikiwa ni ongezeko la Tsh Milioni 600, hii imetokana na
kuongezeka kwa makusanyo ya mapato yetu kutoka Bilioni 119 mwaka 2017/18
hadi kufikia Bilioni 167 mwaka 2018/19” alisema Kindamba.
Kwa
mujibu wa Kindamba alisema TTCL pia imeendelea kusimamia majukumu yake
ya msingi ya ikiwemo kuimarisha mfumo wa viwango vya huduma kwa mteja,
kujenga uwezo wa teknolojia na miundombinu pamoja na kusimamia mkakati
wa mawasiliano kupitia Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa.
Kindammba
anasema katika kuwajengea uwezo vijana katika kujiajiri, TTCL kwa
kushirikiana na Ofisi ysa Waziri Mkuu imeweza kuajiri vijana 50
waliomaliza vyuo vikuu mbalimbali nchini ambao baadae wataweza kuajiriwa
na makampuni mbalimbali ya mawasiliano nchini kwa ajili ya kuongeza
mtandao wa utoaji wa huduma ya mawasiliano nchini.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omary Nundu aliishukuru Serikali
ya Awamu ya Tano kutokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa kwani
katika kipindi cha miaka mitatu, shirika hilo limeweza kupata mafanikio
makubwa kutokana na maono na dhamira ya Rais Dkt. John Magufuli kwa
shirika hilo.
Comments
Post a Comment