Tume
ya Taifa ya chaguzi inapenda kuutaarifu Umma kuwa, haihusiki na
matangazo ya nafasi za ajira yaliyobandikwa katika maeneo mbalimbali ya
Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Matangazo
hayo yanaeleza kuwa, Tume imetoa ajira za muda, na wananchi walioomba
ajira hizo wamekuwa wakiambiwa watoe kiasi cha fedha kwa madai kuwa ni
kwa ajili ya mafunzo.
Hatua
kali za Kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu au kundi la watu wanaotumia
au wanaopanga kutumia jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya vitendo
vya kihalifu.
Tunapenda
kuwashukuru wananchi na kuwasihi kuendelea kutoa taarifa mara tu
wanapohisi uwepo wa watu au kundi la watu wenye nia mbaya ya kulichafua
jina la Tume yaTaifa yaUchaguzi.
Dkt. Athumani Kihamia
MKURUGENZI WA UCHAGUZI
Comments
Post a Comment