Watoto wawili wamepoteza maisha kutokana na athari za mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema
tukio la kwanza lilitokea Mei 8, mwaka huu, saa 9:00 alasiri maeneo ya
Goba wilayani Kinondoni.
Alimtaja
mtoto aliyefariki dunia ni Francis Byabato (6), baada ya kutumbukia
kwenye kisima cha futi 30 kilichokuwa wazi nyumbani kwao.
Alieleza kuwa mtoto huyo alitoweka kwa siku mbili na baadaye alikutwa ndani ya kisima hicho akiwa ameshafariki dunia.
Kamanda
Mambosasa alisema mtoto mwingine ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa
miaka (4-5), alifariki dunia Mei 12, mwaka huu maeneo ya Mongo la Ndege.
Alisema
mwili wa mtoto huyo ulikutwa ukielea katika Mto Msimbazi ukiwa hauna
jeraha lolote na umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kadhalika,
alisema, mvua hizo zinazoendelea kunyesha zimesababisha uharibifu wa
baadhi ya majengo ya Shule ya Msingi Mwale iliyopo Kiwalani, Majani ya
Chai Kiwalani na Shule ya Sekondari Kibasila iliyopo Manispaa ya Temeke
ambayo imejaa maji na kusababisha kushindwa kuendelea na masomo.
Kamanda
Mambosasa alitaja madhara mengine ni kufungwa kwa baadhi ya barabara za
jiji hilo ikiwamo barabara ya Morogoro katika eneo la Jangwani.
Comments
Post a Comment