MHE. BITEKO: VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI HIMIZENI ELIMU






Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoa wa Geita, Doto Biteko na Waziri wa Madini amewaomba viongozi wa madhehebu ya dini kuhimiza waumini wao kusomesha watoto ili kujikomboa na umasikini na kushika nyadhifa mbali mbali za serikali na chama pamoja na uongozi wa dini.
Biteko alitowa wito huo wakati akihutubia mamia ya waumini wa kislamu na wakristo baada ya zoezi la kufuturu pamoja katika ukumbi wa Runzewe Sekondari kata ya Uyovu Tarafa ya Siloka Wilayani Bukombe mkoani hapa. 

Alisema ili kuwa na Taifa bora lazima wazazi na walezi Wilaya ya Bukombe wawekeze kwenye Elimu kwa kushirikiana na viongozi wa madhehebu na tasisi zingine ikiwa serikali imetowa Elimu bure kuanzia darasa la awali hadi kidato cha nne.

“Safu iliyoko meza kuu ipo siku watafika ukomo wa uongozi ikiwemo mimi ili kupata kiongozo bora wanabukombe tuwekeze kwenye Elimu natamani Wakuu wa Wilaya,Wakuu wa Idara kwenye halmashauri mbali mbali nchini, Mikutano ya Kimataifa UN”alisema Biteko. 

“Na umoja wa afirika  Sadek, na nchi zingine za kiafirika miaka kadhaa inayo kuja wawemo watoto kutoka Wilaya ya Bukombe inawezekana, inawezekana maadalizi ya mtoto hayaitaji nafasi au utajili yanaitaji mtoto kutiwa moyo”alisema Biteko.

 
Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hasani Kabeke aliwataka wasilamu kudunisha amani upendo na kushirikiana na wakristo katika kumuabudu mungu katika kweli na kuacha matendo ya siyo mpendeza Mungu.

Kabeke alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Bukombe tangu achanguliwe kuwa Mbunge 2015 na 2016 alianza kufuturisha waislamu hadi leo mwaka wa nne,  sheikh alimuomba Mbunge mwaka wa uchanguzi mkuu 2020 asisite kuanda ftari ya waisilamu na istafasiliwe ni Rushwa.

Akizungumza kwa niamba ya viongozi wa madhehebu ya ki kristo Mwenyekiti wa Parokia ya Bikra Maria Msaada wa Daima Ushirombo Daniel Lutonja  alisema mbunge huyu amekuwa akifanya jambo jema la kuwa na mahusiano ya madhehebu ya dini.

Lutoja aliwaomba wananchi kila mtu kwa imani yake kuendelea kumuombea mbunge na viongozi wenzake akiwemo Rais John Magufuli kwa kazi kubwa wanazozifanya. 



Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba aliwatakia waislam wote mfungo wa ramadhani mwema na maandalizi mema ya sikuku ya kufungua ambayo kama haitabadilika karenda itakuwa Juni 4 au Juni 5 mwaka huu.

Nkumba alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya imejipanga vema kuhakikisha sherehe za waislamu wanasherekea kwa amani na yeyote atakae fanya fujo atachukuliwa hatua kali za kisheria.






 



Comments