KILA HALMASHAURI ZA MKOA WA GEITA KUANZA KUJENGA MASOKO YA DHAHABU


Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robart Gabriel akizungumza na wakazi wa Uyovu Wilayani Bukombe.

Meza kuu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robart Gabriel




Halmashauri sita zinazounda Mkoa wa Geita, kuanza kujenga masoko ya dhahabu ili wachimbaji wadogo wadogo na wananchi wengine kunufaika na madini ya dhahabu yaliyopo chini ya Ardhi ya Mkoa wa Geita.

Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robart Gabriel akiwa kata ya Uyovu Wilayani Bukombe wakati wa ziara ya kwenda anasikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Alisema kutokana na upatikanaji wa dhahabu katika makusanyo ya kodi mwaka jana amekusanya sh bilioni 11 toka mgodi mmoja kwa mwaka baada ya kubana mianya ya rushwa na utoloshaji wa madini.

Gabriel alisema kupitia soko la dhahabu lililofunguliwa mwaka jana mkoani hapa serikali imepata sh 20 bilioni kutokana na kudhibiti mianya ya utoloshwaji wa madini.

Na kwamba kuna fedha nyingine sh bilioni 11 iliyopatikana kwa mwaka jana kutoka mgodi wa GGM  kufatia hali hiyo itanufaika na fedha hizo ikiwemo Bukombe imetengewa sh milioni 100 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ili kubadilisha sura ya Mkoa wa Geita na mei mwaka huu atafungua soko la dhahabu na kila Wilaya itakuwa na soko la dhahabu.

Aliwataka watumishi wa umma kuwa waadilifu kwa fedha za serikali ikiwa hapo nyuma Mkoa wa Geita ilikuwa nyuma kutokana na viongozi wa serikali na watumishi wengine wa chini walikuwa sio waminifu na walipenda Rushwa.

Miradi ya maendeleo katika idara ya Elimu vyumba vya madarasa 2500 vimekamilika kwa mwaka 2018 na zahanati  wakati anakuja Mkoani hapa kulikuwa na asilimia 25 tu ya miundo mbinu ya zahanati leo kila kijiji kuna maboma na kufikisha asilimia 66.5 uboreshaji wa miundombinu ya afya na ifikapo 2021 hakuna kuzungmuzia upungufu wa madarasa wala matundu ya vyoo lengo la serikali kusogeza huduma ya Afya kwa wananchi.

Gabriel alisema uchumi wa Geita unapatikana kutokana na dhahabu na malengo ya serikali ya Mkoa ni kujenga kijiji cha Uchumi na tayari zimetengwa hekari 100 na tasimini ya michoro imekamilika baada ya maoyesho ya kitaifa mwaka huu Dar es Salaam  Geita itapokea watu wa kigeni kwenye maonyesho ya dhahabu kimataifa ikiwa  Mkoa wa Geita uko katikati ya Umoja wa Afirika Mashariki.

Samson Jeremia aliipongeza serikali ya Mkoa kwa makusanyo ya fedha na kwamba serikali itakapo jenga soko la dhahabu Bukombe watanufaika zaidi.

Juma Yusuph alisema alikuwa hajui kama Geita inautajili aliomba serikali kubadilisha mazingira ya kila Wilaya ili wananchi waendelee kunufaika na miradi itakayoletwa na serikali ya Mkoa.

Comments