
Mbunge
wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu,ametoa ahadi ya kuhakikisha kuwa miradi ya
maendeleo itakayotekelezwa mwakani katika Halmashauri ya Mji wa Geita
itazingatia taratibu zote zinazotakiwa ili isiweze kukataliwa.
Kauli
hiyo imekuja mara baada ya mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu
kubaini baadhi ya kasoro katika miradi iliyotekelezwa katika Halmashauri
hiyo hali iliyolazimu mradi wa maji kushindwa kuzinduliwa.
Hayo
ameyasema wakati alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kasamwa katika
eneo ambalo mkesha wa Mwenge ulipofanyikia katika Halmashauri ya Mji wa
Geita mkoani Geita.
Kufuatia
hali hiyo ya mradi wa maji kushindwa kuzinduliwa unaodaiwa kugharimu
shilingi bilioni sita, hali hiyo imempelekea Kiongozi wa mbio za
Mwenge wa mwaka huu, Mzee Mkongea Ally kuiagiza Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa kuchunguza mradi huo .
Mhe.Kanyasu
amesema mwaka huu ukimbizaji Mwenge umekuwa na maana kubwa kufuatia
kufanya ukaguzi usiotia shaka kwenye miradi iliyotekelezwa na pale
wanapobaini ukiukwaji miradi hiyo imekuwa haizinduliwi.
"
Ukaguzi mnaoufanya katika miradi hii ni ishara tosha kabisa kuwa
mmekuja kufanya kazi kwa ajili ya wananchi'' alisisiiza Kanyasu
Amesema
miaka ya nyuma zoezi la ukimbizaji Mwenge lilikuwa la kawaida hali
iliyopelekea kila miradi iliyotekelezwa kuzinduliwa bila kujalisha
thamani ya pesa inayoendana na miradi halisi.
"
Mimi binafsi niliweza kupata bahati ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru hapo
nyuma kidogo, Tulikuwa hatufanyi ukaguzi makini kama unaofanyika mwaka
huu.
Akizungumzia
kuhusu kasoro zilizojitokeza katika miradi ya mwaka huu, Mhe.Kanyasu
amesema kasoro zote zilizojitokeza mwaka huu hazitajirudia katika
Halmashauri hiyo, hivyo ameahidi kuzifanyia kazi.
Katika
hatua nyingine, Mhe, Kanyasu amesema mkoa wa Gieta ni nyumbani kwa
Mhe, Rais, Joseph Pombe Magufuli hivyo mwaka ujao atahakikisha hakuna
miradi wowote utakaotaliwa kwa vile ni aibu kwao.
Comments
Post a Comment