ILEMELA- Zahanati ya Lukobe kuleta ahueni kwa wananchi



Kukamilika kwa ujenzi wa Zahanati ya Lukobe iliyopo Kata ya Kahama wilayani Ilemela, kunatarajia kuleta ahueni ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa Mtaa wa Lukobe ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu hadi kilomita 10 kusaka huduma za afya.

Mradi huo uliofunguliwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa jumapili Mei 19, 2019 ni miongoni mwa miradi 10 iliyopitwa na Mwenge wilayani Ilemela ambapo ujenzi wake ulianza baada ya kuibuliwa na wakazi wa Mtaa wa Lukobe na kuungwa mkono na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela pamoja na mfadhili kutoka nchini Canada, Dawn Shaller.

Comments