
Takribani
watu 156 wanaripotiwa kufariki dunia na mamia kujeruhiwa kufuatia
milipuko iliyotokea katika makanisa na hoteli nchini Sri Lanka.
Milipuko
sita imeripotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali nchini humo wakati
raia wa nchi hiyo wakisherehekea sikukuu ya Pasaka.
Katika
milipuko hiyo sita iliyotokea, milipuko mitatu imetokea katika
makanisa, huku mingine mitatu ikitokea katika hoteli tatu tofauti.
Makanisa
ambamo milipuko imetokea ni Kochchikade, Negombo na Batticaloa huku
hoteli zilizokumbwa na milipuko zikiwa ni, The Shangri La, Cinnamon
Grand na Kingsbury.
Picha
mbalimbali katika mitandao ya kijamii zinaonesha hali ilivyo katika
baadhi ya maeneo ambamo milipuko hiyo imetokea. Majengo yanaonekana
yameharibika, pamoja na damu za watu kutapaa chini, huku vyombo vya
huduma ya kwanza na Polisi wakitoa misaada.
Rais
Maithripala Sirisena amewataka wananchi kuwa watulivu wakati wa kipindi
hiki kigumu, na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi ili kufanikisha
uchunguzi.
Viongozi
wengine nchini humo wamelaani mauaji hayo ambayo yanayoonekana kuwa
yalikuwa yamepangwa, na kugharimu uhai wa watu wasio na hatia.
Comments
Post a Comment