Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi
Lugola ametembelea na kukagua ujenzi wa nyumba za makazi ya askari
polisi zinazojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini
Shinyanga na kushangazwa na kasi ya ujenzi na matumizi kiasi kidogo cha
fedha tofauti na jinsi ilivyotarajiwa.
Lugola amejionea hali ya ujenzi huo jana
jioni Alhamis Aprili 18,2019 ambapo ujenzi huo unatokana na fedha
shilingi milioni 225 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Awali akitoa taarifa,Mwenyekiti wa
kamati ya ujenzi huo, Inspekta Cosmas Peter Taligula alimweleza Waziri
Lugola kuwa ujenzi ulianza Februari 28,2019 na unatarajiwa kumalizika
mwezi June mwaka huu na mpaka sasa wamefikia asilimia 75 ya ujenzi.
“Katika ujenzi huu tunashirikiana na
Magereza na VETA na tunatumia ‘Local Fundi’,hadi sasa tumetumia shilingi
milioni 118, zilizobaki benki ni milioni 107,tunajenga nyumba 10 badala
ya 9 zilizopo kwenye mpango”,alieleza Taligula.
“Hizo nyumba 9 zilitakiwa kuwa na
vyumba viwili vya kulala,jiko,choo na bafu lakini sisi tunajenga nyumba
10 zenye vyumba vitatu vya kulala ‘kimoja kikiwa ni master
room’,jiko,bafu na choo na tunatarajiwa kukamilisha ujenzi mwezi June
mwaka huu”,aliongeza Taligula.
Baada ya kukagua ujenzi huo,Waziri
Lugola alieleza kushangazwa na kazi nzuri inayofanywa na kamati hiyo ya
ujenzi huku akisema kama wangetumia wakandarasi kwenye ujenzi huo huenda
zingetumika hata zaidi ya shilingi bilioni moja mpaka sasa.
“Nimeridhishwa na kasi yenu na
ubunifu wenu,Mimi kama Waziri nimetembelea miradi mingi,hapa nimekuta
vitu vya ziada,nimejifunza mambo mengi, wameongeza idadi ya majengo
kutoka lakini pia wamepanua ukubwa wa eneo kwa fedha zile zile shilingi
milioni 225 tena wamejenga majengo ya kiwango na ya kisasa ”,alieleza Lugola.
“Nitashauriana na IGP Simon Sirro
nimuombe kamati hii iwe ya mfano ,kamati hii itembelee maeneo mengine
nchini iwaeleze uzoefu wa kujenga nyumba za kisasa na kwa gharama nafuu
kwani hii itatusaidia kujenga nyumba nyingi za makazi ya askari wetu”,alisema Lugola.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi
Lugola akisalimiana na maafisa wa jeshi la polisi alipowasili jana jioni
kutembelea na kukagua ujenzi wa nyumba za makazi ya askari polisi
zinazojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi huo, Inspekta Cosmas Peter Taligula
(kulia) akimweleza Waziri Kangi Lugola kuhusu ujenzi wa nyumba za makazi
ya askari eneo la Kambarage Mjini Shinyanga.
Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi huo, Inspekta Cosmas Peter Taligula akiendelea kuelezea kuhusu ujenzi huo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiupongeza uongozi wa
jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kusimamia ujenzi wa nyumba za
makazi ya askari polisi.Aliipongeza kamati ya ujenzi kwa kuwa wabunifu
na kujenga majengo ya kisasa kwa gharama nafuu.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao akielezea
namna jeshi la Magereza na Chuo cha Ufundi Stadi VETA wanavyoshirikana
nao katika ujenzi wa nyumba za makazi ya askari polisi.
Muonekano wa nyumba za makazi ya askari polisi zinazojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Muonekano wa jengo la nyumba za makazi ya askari polisi zinazojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao (kushoto)
akimwongoza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kukagua
ujenzi wa nyumba za makazi ya askari polisi zinazojengwa katika eneo la
Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao (kushoto)
akimwongoza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kukagua
ujenzi wa nyumba za makazi ya askari polisi zinazojengwa katika eneo la
Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akikagua moja ya majengo hayo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiendelea kukagua majengo hayo.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao akionesha
nyumba zinazoendelea kujengwa katika eneo la Kambi ya jeshi la polisi
Kambarage.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiondoka katika eneo la
ujenzi wa nyumba za makazi ya askari Kambarage mjini Shinyanga jana
majira ya saa moja na dakika 45 usiku.
Comments
Post a Comment