
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amezionya na
kuzitaka Taasisi za Uhifadhi kuacha tabia ya kuwabughudhi wananchi
wanaoishi katika vijiji na vitongoji 366 vilivyokutwa ndani ya Hifadhi
katika maeneo mbalimbali nchini mpaka hapo maamuzi ya Kamati ya Mawaziri
saba iliyoundwa kushughulikia suala hilo itakapokamilisha kazi
iliyopewa na kuwasilisha ripoti kwa Mhe. Rais.
Hatua
hiyo ni kufuatia malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wakiwemo
wakulima na wafugaji wanaoishi katika vijiji na vitongoji hivyo kudai
kuwa wamekuwa wakisumbuliwa na mifugo yao kukamatwa mara mara kwa madai
ya kukutwa imeingia ndani ya Hifadhi.
Akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Kisondoko ambacho ni miongoni mwa vijiji
vilivyomo ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero katika wilaya ya Kondoa
mkoani Dodoma, Mhe. Kanyasu amezitaka taasisi hizo kufuata na
kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Serikali kuhusu wananchi wanaoishi
katika maeneo hayo.
Aidha,
Mhe. Kanyasu ametumia fursa hiyo kuwaonya wananchi ambao wamekuwa
wakivamia maeneo mapya ya Hifadhi kwa kisingizio cha kauli aliyoitoa
Mhe. Rais kuacha mara moja na kwamba yeyote atakayekamatwa hatua kali
za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
"
Wananchi ninao walenga ni wale tu ambao walikuwa wakiishi Hifadhini
kabla ya kauli ya Rais aliyoitoa mwanzoni mwa mwaka huu" Alisisitiza.
Hata
hivyo, Mhe Kanyasu amebainisha kuwa Kamati ya Mawaziri saba iliyoundwa
na kuzunguka nchi nchi nzima imebaini kuwa kuna zaidi ya vijiji 820
ambavyo vimo ndani ya Hifadhi mbali ya vile 365 vilivyobainishwa awali
na kuwasihi wananchi wasiendelee kuvamia maeneo mengine.
Mhe.Kanyasu
ameowanya baadhi ya askari wa wanyamapori wanaoomba rushwa Kutoka kwa
wafugaji pindi wanapokamata mifugo yao ili waweze kuiachia waache mara
moja tabia hiyo akisisitiza kwamba askari yeyote atakayethibitika
atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria za utumishi wa
Umma.
Mkuu
wa wilaya ya Kondoa, Mhe. Sezaria Makota amewataka wananchi hao
kuendelea kuwa walinzi wa maeneo hayo huku wakisubili hatma ya taarifa
ya kamati ya Mawaziri saba itakayotolewa hivi karibuni.
"
Baada ya taarifa hiyo mtajua hatma yenu na kama hapa mtabaki au
mtahamishwa na kama mtahamishwa tutajua tutawapeleka eneo gani kwa ajili
ya malisho na kilimo." Alisema.
Akizungumza
kwa niaba ya Wananchi, Mwenyekiti wa kijiji cha Kisondoko, Ismail Said
amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa baadhi ya askari wa wanyamapori
wamekuwa wakikamata mifugo yao na kuomba rushwa na pale makubaliano
yanaposhindikana huondoka na mifugo yao.
Comments
Post a Comment