Majeshi ya majini ya Iran na Urusi yanapanga mazoezi ya pamoja na ya kipekee katika Ghuba ya Uajemi baadaye mwaka huu.
Hayo
yametangazwa na Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran Admeri Hossein Khanzadi ambaye ameyadokeza hayo alipozungumza na
waandishi habari mapema leo mjini Tehran baada ya kurejea kutoka China
ambapo amekutana na makamanda wenzake kutoka kote duniani.
Admeri Khanzadi ameongeza kuwa, tayari mazungumzo yameshaanza na Urusi kuhushu maozeozi hayo ya pamoja.
Majeshi
ya majini ya Iran na Urusi hufanya mazoezi ya pamoja mara kwa mara
katika Bahari ya Kaspi na kwa msingi huo mazoezi yajayo katika Ghuba ya
Uajemi yatainua kiwango cha uhusiano wa pande mbili.
Admeri
Khanzadi aidha ameashiria mpango wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa
kuimarisha uhusiano wa mafunzo na majeshi ya majini ya nchi zingine na
kusema: "Iran inachunguza mwaliko kutoka nchi kama vile India, China,
Pakistan na Italia ambazo zimetaka ushirikiano katika mafunzo kwa
maafisa wa kijeshi."
Kamanda
wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria matamshi
ya hivi karibuni ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel ambaye
alitishia kuzishambulia meli za mafuta za Iran na kusema "maji ya
kimataifa ni ya nchi zote, na hivyo jeshi la majini lina jukumu la
kulinda maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."
Admeri
Khanzadi amesisitiza kuwa, meli za mafuta za Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran ni sehemu ya ardhi ya nchi hii na zitalindwa kikamilifu.
Comments
Post a Comment