IMF: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran vinavuruga ukuaji wa uchumi katika eneo la Mashariki ya Kati
Shirika
la Fedha Duniani (IMF) limesema leo kwamba vikwazo vya Marekani dhidi
ya Iran, kuongezeka kwa machafuko katika Mashariki ya Kati na Afrika
Kaskazini na tatizo la bei ya mafuta vinadhoofisha ukuaji wa kiuchumi
katika kanda hiyo.
Mkurugenzi
wa IMF wa Idara ya Mashariki ya Kati na ya Asia ya Kati, Jihad Azour,
amesema hali hiyo pia inachochea ukosefu wa ajira katika kanda hiyo.
"Kasi
ya polepole ya ukuaji wa uchumi inazua kutengenezwa ajira
zinazohitajika ambazo zitawawezesha kupunguza kiwango cha ukosefu wa
ajira. Katika miaka mitano ijayo, kanda hiyo inahitaji kuunda nafasi
mpya za kazi zaidi ya milioni 25, ili kuimarisha kiwango cha ukosefu wa
ajira kinachoshuhudiwa sasa katika kiwango cha juu," amesema Jihad
Azour.
Shirika
hilo linatabiri uchumi wa Iran, ambao ni wa pili kwa ukubwa katika
kanda hiyo baada ya Saudi Arabia, utaanguka kwa asilimia 6.0 mwaka huu
baada ya kupungua kwa asilimia 3.9 mwaka 2018.
Uchumi
wa Iran umeanza kuporomoka baada ya Marekani kuamua kuiwekea tena
vikwazo nchi hiyo, kufuatia Rais Donald Trump kujitoa katika makubaliano
ya silaha za nyuklia ya mwaka 2015.
Comments
Post a Comment